Mkutano wa 10 wa Kamati za Bunge za Hesabu za Serikali kutoka Mabunge ya Nchi wananchama wa SADC ujulikanao kama (SADCOPAC) unaendelea jijini Arusha, ambapo kamati ya Bunge ya PAC ndio mwenyeji wa Mkutano huo.
Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) Mhe. Zitto Kabwe akiwasilisha Taarifa ya Tanzania ya utekelezaji wa Maazimio ya Mkutano wa 8 na 9 ikiwa ni matakwa ya Wajumbe wa Mkutano huo ambapo kila Nchi wanachama huwasilisha taarifa hiyo.
Mjumbe wa Mkutano wa Mwaka wa SADCOPAC kutoka Tanzania Mhe. Asumpta Mshama akiuliza swali wakati wa majadiliano ya mkutano wa Umoja wa Kamati za Bunge za Hesabu za Serikali kutoka nchi zilizo kusini mwa jangwa la sahara (SADCOPAC) unaoendelea Arusha. Tanzania imewasilisha utekelezaji wa maazimio ya mikutano ya 8 na 9 katika mkutano huo.
Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) Mhe. Zitto Kabwe akimweleza jambo Mwenyekiti wa Umoja wa Kamati za Bunge za Hesabu za Serikali kutoka nchi zilizo kusini mwa jangwa la sahara (SADCOPAC) ambaye pia ni mwenyekiti wa PAC kutoka Bunge la Afrika Kusini Mhe. Sipho Makama wakati wa mapumziko ya Mkutano wa 10 wa SADCOPAC unaendelea Arusha.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Bravo Zotto. May God Bless you!

    ReplyDelete
  2. hongera zitto. Mwenyezimungu atakulipa kheri.

    ReplyDelete
  3. MSHIKAJI ZITTO MBONA KAKITAMBI KAKAANZA TARATIBU? WEWE BWANA MTU WA KILEO EMBU NJOO HUKU GYM UUNYOSHE MWILI USIWE KAMA KINA MWANA FULANI,

    UNCLE SA, LAKINI ALL THE BEST BRO! MPAKA KIJULIKANE

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...