![]() |
Baadhi ya vijana wanaodai kuwa wanatoka mkoa wa Kigoma wakiwa wajaza fomu leo ambao taarifa zao zinaendelea kuchunguzwa kama kweli ni Watanzania wakiwa katika Ofisi ya Uhamiaji Mkoa wa Dares Salaam. |
![]() |
Gari la Idara ya Uhamiaji likiwa limebeba baadhi ya watuhumiwa hao mara baada ya kutoka mahakamani. |
NA MAGRETH KINABO
– MAELEZO
OFISI ya Uhamiaji mkoa wa Dares Salaam imemfikisha mahakamani Mtanzania anayedaiwa kuwatunza raia watano kutoka Nigeria wanaoishi nchini bila kibali halali baada ya kuwapiga na kuwazuia kufanya kazi maofisa wa uhamiaji kwenye ofisi za Serikali.
Hayo yalisemwa leo na Ofisa wa Uhamiaji wa Mkoa wa Dares Salaam, Grace Hokororo wakati akizungumza na mwandishi wa Idara ya Habari –MAELEZO ofisini kwake ambapo alisema Mtanzania huyo alifikishwa leo(jana) katika mahakama ya Hakimu Mkazi ya Kisutu baada ya kutenda kosa hilo jana majira ya saa 1:00 jioni.
Alimtaja Mtanzania huyo kuwa ni Christopher Kanyala mwenye umri unaokadiriwa kuwa kati miaka 29 hadi 34 mkazi wa Sinza na anadaiwa kuwa aliwaHI kutumikia Jeshi la Polisi nchini, ambapo kesi yake na raia hao watano wa Nigeria itatajwa kesho katika mahakama hiyo.
Akizungumzia kuhusu suala hilo , Grace aliwataka wananchi wasipende kuishi na raia ambao ni wageni na hawajaripoti katika ofisi za uhamiaji kwa kufanya hivyo ni kosa kisheria. Huku akiwataka raia wa kigeni kuripoti katika ofisi hizo mara baada ya kuwasili nchini ili waweze kufuata taratibu za kisheria.
Aidha alisema operesheni ya kuwakamata wahamiaji haramu inaendelea vizuri. Grace alisema kwa upande wa wahamiaji haramu kutoka Malawi walijitokeza kwa hiari mpaka leo mchana idadi yao imefikia 1,863 tangu zoezi hilo lilipoanza.
Aliongeza kuwa opresheni hiyo imehusisha mataifa 31 ambapo alitaja baadhi yake kuwa ni Kenya, Uganda, Burundi, Rwanda,Italia, Singapore Ethiopia,Libya Yemeni,Somalia,Komoro, Ujerumani, Afrika Kusini,Uturuki, Nigeria, Cameroon,Liberia na Bokinafaso., Jamhuri ya Kidemkrasia ya Kongo(DRC) na India.
Alisema jumla ya raia hao wa mataifa mengine waliokamatwa ni 502.
Mbona Blogger umempa jina la Mwinjilisti MWANAMKE..? Jina lake lilikosekana kabisa?
ReplyDeleteKick her and the people she has been harbouring out NOW!
ReplyDeleteHongera Uhamiaji kwa kazi nzuri, nchi yetu imejaa raia wa nje wasio na vibali,wakati huo huo sisi watanzania husumbuliwa sana na mambo ya vibali tunapokuwa ugenini,Sana sana huishia kusafirishwa kama mbwa. Sasa na sisi inabidi tuwe wakali na nchi yetu. Watu kama wa Nijeria wanapitia ktk visingizio vya dini huku wanauza madawa ya kulevya pia kupata passport zetu na kwenda kuzifanyia uhalifu nje. Wasakwe wote pia wafadhili wao wahukumiwe, Tusifanye makosa hata siku moja kuwa amini wa Nijeria ambao wame kwisha shindikana dunia nzima,Wanafanya Tanzania ndio kichaka cha kupitia, Serikali Iwe macho sana na watu hawa waendelee kusakwa mpaka waishe wote,wasiachiwe nafasi hata kidogo,Kama ni huduma za kanisa wapeleke kwao
ReplyDeleteNdio muone sasa athari za kukosa somo la uraia, hata uzalendo hakuna.Binafsi nimeishi Ukraine mda mwingi, nimeshuhudia jinsi wananchi wao walivyo makini kuwagundua watu wasio raia na mara moja huwatonya polisi,vilevile polisi nao huko mtaani ndio usiseme, kila baada ya mita 20 unaulizwa documents, vilevile hata kama utafanikiwa kuishi kinyemela bado maisha yatakua magumu kwani hata kuuza karanga hutoweza,sembuse kufanya kazi ya kuhubiri, kwakua mfumo wao jinsi ulivyo ni lazima ukaguliwe na taarifa zako ziwe zinapelekwa juu mara kwa mara.
ReplyDeleteCommoditization of Religion na manabii fake!
ReplyDeleteMliokuwa mna abudu katika jumba hilo, nanyi mmeshiriki katika kufuga maharamia hawa. Mlikuwa nanashiriki katika dhambi. Ni muda muafaka wa kukiri na kumrejea Yesu kwa dhati.
Great job immigration!!!! Kick them out of our country! And the Nigerian mchingaji, arudishwe kwao pia! Mtu mwema anapo muhifadhi muhalifu na yeye ni mwalifu kwa Nokia moja au nyingineeee. Watanzania wrnzangu tuendelee kuwafichua wageni Woote walio nchini kinyuma cha Sheria. Na passport za Tanzania ziangaliwe pia! Wengi wanafanya uhalifu kwa kutumia passport zetu Za Tanzania na wao si watanzania!
ReplyDelete