
Meneja wa Tanroads wa mkoa wa Iringa Injinia Poul Lyakurwa
alimtaarifu Waziri Magufuli kuwa kiasi cha Shilingi milioni 31.9 kilikusanywa
katika kipindi hicho cha mwezi mmoja.
Akishitushwa na kiwango hicho Waziri Magufuli alibainisha kuwa, kiasi hicho kilichosomwa
katika taarifa kimetokana na magari 735 yaliyokamatwa kati ya magari 20,700
yaliyopimwa sawa na asiliamia 3.5.
“Takwimu hizi sizikubali kwani wastani wa
magari yanayokamatwa katika nchi nzima unakaribia asiliamia 40 iweje barabara
kuu kama hii iwe na kiwango kidogo kiasi hicho cha magari yaliyokutwa na makosa”
hapa ni lazima pafanyike uchunguzi” alisisitiza Mheshimiwa Magufuli na kueleza
kuwa hali hiyo hawezi kuiruhusu hata kidogo kuendelea.
Katika hatua nyingine
Waziri Magufuli amempongeza Meneja huyo wa Tanroads kwa kufukuza wafanyakazi 18
katika Kituo cha Mizani cha Makambako kwa kutokuwa waaminifu katika kazi zao. Waziri
huyo wa Ujenzi aliendelea kubainisha kuwa, takriban asilimia 70 ya wafanyakazi
waliokuwa katika vituo mbali mbali vya mizani ya barabara nchi nzima wamebadilishwa
baada ya kukamilika kwa zoezi la kutangaza nafasi hizo upya.
Akisisitiza zaidi, Waziri Magufuli alisema “Wizara ya Ujenzi
itaendelea kushirikia na taasisi mbali mmbai zikiwemo PCCB, Jeshi la Polisi,
TRA na hata kwa kutumia makondakta na wasaidizi katika magari ya usafirishaji
ili kuendelea kubaini mbinu mbali mbali ambazo zinaendelea kutumika katika
suala zima la vitendo vya rushwa katika vituo vya mizani hapa nchini”.
Kwa upande mwingine Wakala wa Majengo Nchini pamoja na
Wakala wa Ufundi na Umeme wametakiwa kuwa wabunifu ili waweze kukabiliana
kikamilifu na changamoto mbali mbali zinazowakabili.
Hili ndio tatizo kubwa alilonalo huyu waziri. Haimuingii akilini hata kidogo kuwa wasafirishaji wamebadilika na hawazidishi uzito na kauli hizi ndio hua zinawafanya wafanyakazi wa mizani wawaonee wamiliki wa magari
ReplyDelete