Ile operesheni ya kuwatimua wahamiaji haramu nchini Tanzania imeanza kutekelezwa ambapo juzi na jana, watu 1851 walikamatwa katika mikoa ya kandoni mwa maziwa Nyanza na Tanganyika ndani ya siku moja.


  • Operesheni hiyo  pamoja na mengine inalenga kufukuza majambazi, majangili, pamoja kukamata silaha zinazosadikiwa kutumika katika matendo ya kihalifu nchini.  Baadhi ya watu walisalimisha silaha zao huku wengine wakiziacha kwa wenyeji.



Mkuu wa Operesheni hiyo kubwa kuliko zote zilizowahi kufanyika nchini Tanzania, iliyopewa jina la,


“Operesheni Kimbunga”, Naibu Kamishina wa Polisi, Simon Sirro amewaasa wananchi kuwa makini na ‘kurithishwa’ silaha hizo kwani  ni kinyume na sheria na inawezekana silaha hizo zikawa zimehusika katika vitendo vya kihalifu na hivyo kumsababishia ‘mrithi’ kushitakiwa kwa mujibu wa sheria.



Kuhusu malalamikao ya kutengwa kwa familia za baadhi ya wenyeji na wahamiaji waliooana, Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Kanali mstaafu Fabian Massawe amesema wengi wa walioondoka kwa hofu hawakuwa na ufahamu kuhusu sheria na hivyo amewataka kuwafike kwenye ofisi za Uhamiaji ili wapatiwe hati za utambulisho na kuishi nchini zitakazotumika kwa muda wa miaka 2 wakisubiri taratibu za kuwapatia uraia.



Mwezi Julai tarehe 29, Rais Kikwete alitoa wito kwa wahamiaji wote haramu waondoke nchini ndani ya siku 14 ambapo ilitarajiwa wangeondoka zaidi ya 50,000 lakini hadi sasa wameondoka 11,600 tu.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. Hiki kimbunga kifanyike nchi nzima ili tutoe majangili wote nchini mwetu,dar ndio usiseme mikenya minaigeria,mikongo,mighana,mirundi,midosi,waarabu koko,mipakistani,mibangradeshi,

    ReplyDelete
  2. Ubaguzi. Unajuwa hata wale raia watokao mikoa ya mpakani hupata shida kwa kushukiwa wakimbizi na kutakiwa kuthibitisha uraia wao. Tena hukuti viongozi wa juu wa serikali/jeshi nk. wakitokea huko.

    Watokao mikoa mengine shwari.

    Kuacha ubaguzi sakeni mikoa yote. Pia wanaweza kujificha mikoa msiosaka.

    ReplyDelete
  3. YAANI HICHO KIMBUNGA KISIMUACHE MTU, HASA DAR ES SALAAM NDIO INA NUKA KWA UJANGIRI NA WENGI WANAOUA NI WAGENI WANAOTUMIWA NA WENYEJI.
    WARUNDI,WAKENYA,NIGERIANS,PAKISTANS AMBAO NDIO WALETAJI WA MAUNGA YOTE HAPO TANZANIA HALAFU KUWAPATIA WATANZANIA WASIOKUWA NA HATA IDEA OF WHAT IT IS. SEREKALI IWAANGALIE SANA HAO ASINS NI WASHENZI SANA NA MICHORO HIYO YA MAUNGA NA HAPO NDIO WANASAFIRISHA KWENDA NCHI ZINGINE KWA KUWATUMIA VIJANA WA KITANZANIA KWA KUSAFIRISHA BIASHARA YAO, HALAFU PESA ZOTE ZINAENDA WANUFAISHA AL QAIDA

    ReplyDelete
  4. We anon wa 3 toa ushahidi wa hao unaowatuhumu na kwamba pesa inakwenda Alqaida

    ReplyDelete
  5. Serikali sasa ni Mkali kama baba!

    Jamaa wamepeta sana na sasa kiama kinawashukia, ilikuwa ukiwa na suala lako kwa Mgeni hasa Wahindi, unakuta Mgeni anakutunishia kifua Mwenyeji ana kwambia ''CHACHA WEYE MIMI KUBA YAKO IKO KENE KONO YANGU, WEWE NASEMA NINI APA?''

    Jeuri hiyo sasa hakuna wanakabiliana na Kimbunga !!!

    ReplyDelete
  6. Madiaspora Majuu!

    Madiaspora Majuu!

    Maiaspora Majuu!


    Tanzania sasa kama Majuu!!!

    Na sisi tunawatoa nduki Wahamiaji haramu kama ninyi ndugu zetu mnavyo fanyiwa huko Majuu, maana wamekuja kula nchi Bongo kama wapo kwao vile?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...