Ankal salama?
Naomba unisaidie msaada tutani. 
Niulizie kwa wadau je ni mkono upi unaofaa kuvaliwa saa ya mkononi?
Nauliza hivyo kwa sababu juzi juzi nimenunua bonge moja la saa na kuivaa mkono wa kulia. 
Mai waifu wangu na majamaa kibao wakanicheka sana kuwa mwanaume anatakiwa kuvaa saa mkono wa kushoto. Nilipoenda kazini kuna waliosema mkono wa kulia unafaa na wengine wakabakia kudai kwa mwanaume ni mkono wa kushoto na kwa mwanamke ni mkono wa kulia. Yaani nimechanganyikiwa. 
Ati jamani  wadau nivae saa yangu mkono upi na kwa sababu gani?

Ni hayo tu Ankal
Email yangu kapuni maana najua 
nitazodolewa hapa hadi nikome...

Mdau Unyamwezini

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 12 mpaka sasa

  1. Acha kutuzuga bwana,tuzungumzie msala wa katiba mpya kwanza.

    ReplyDelete
  2. Una mikono miwili? the choice is yours.Unajua watu wengi ni right handed, na mkono wa kulia una kazi zaidi na shock kila unapofanya kazi. Saa za awali zilikuwa si shock proof, basi zilikuwa na maisha marefu zaidi zikivaliwa kwenye mkono wa shoto.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Swadakta vaa wewe na nafsi inavyopenda la sivyo utakosolewa mengi kwenye hii Dunia, kuna Wanavaa kulia sababu akiendesha gari usikani upande mwengine anaogopa kuporwa dirishani na wezi, kuna watu wana Imani za Dini wanavaa kitu kama hilo mkono wa Kulia kuliko Kushoto ila ukitaka kuiga ya West mengine yatakutoka Puani, Mie navaa mkono wa Kulia na atayesema Mwanamke anavaa wa Kulia na aseme mie najijua ni Mwanaume na Mungu alieniumba anajua hilo linatosha wasikuumize kichwa kama Mdau juu kasema Saa ni yako Kushoto sawa na Kulia sawa.

      Delete
  3. Uamuzi wako, lakini kama wewe ni muislam tumia wa kulia ni sunna hata mtume wetu alikuwa akitumia wa kulia.

    ReplyDelete
  4. Ulizeni maswali ya maana yaani hata kuvaa saa unataka uelimishwa!!!mbona utaelimishwa mengi. Eti umechanganyikiwa mwanaume unatia aibu, inamaana ndo Mara ya kwanza kwako kuvaa saa? Majanga

    ReplyDelete
  5. Muulize muuzaji wa hiyo saa uivaliye mkono gani?

    ReplyDelete
  6. Mkuu uamuzi wako jinsi ya kuvaa saa mkono wa kulia si tatizo vaa tu,mbona mwalim nyerere alikuwa anavaa kulia

    ReplyDelete
  7. Vaa kiunoni! Mkono ni mkono tu!

    ReplyDelete
  8. Kuna 'unwritten/general rule' kwamba inategemea na mkono wako unaitumia kuandika i.e. kulia ama kushoto na kwa hiyo uvae kinyume chake. Mfano uko right handed, uvae mkono wa kushoto. Hii, pia itapunguza uzito wakati wa kuandika. Lakini, la msingii, uamuzi ni wako. Excellent example ni Rais wetu, ambae nimemwona yuko right handed na mara nyingine huwa anavaa saa mkono wake wa kulia. Hope this helps.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...