Mkongwe
wa muziki wa kizaz kipya a.k.a Bongofleva Afande Sele a.k.a Baba Tunda
a.k.a Simba Mzee akidhihirisha ukongwe juu ya steji ya tamasha la
Serengeti linalofanyika usiku huu ndani ya uwanja wa Jamuhuri mkoani
Dodoma,ambapo maelfu ya watu washabiki wamejitokeza kushuhudia tamasha
hilo ambalo hufanyika mara moja kwa mwaka.
Msanii
mahiri ambaye kwa sasa anasumbua vilivyo anga ya muziki wa
Bongofleva,Diamond akiwaimbisha mashabiki wake usiku huu kwenye tamasha
la serengeti fiesta 2013,linalofanyika usiku huu kwenye uwanja wa
Jamuhuri.
Haaaa
haaaa...ukitaka kubana pua kabane nyumbani kwenu,hapa ni hip hop
tuuu.....Msanii wa Bongofleva Ney wa Mitego wakioneshana umahiri umwamba
wa jukwaani na msanii mwenzake Dimond kupitia wimbo wa Muziki Gani.
Maelfu ya Watu wakiwa kwenye uwanja wa jamuhuri,usiku huu wakishangweka na tamasha la Serengeti Fiesta 2013.
Mwanadada ambaye wengi wanadai amerithi viuno na sauti kutoka mwanamuziki Ray C,anaitwa Rachael kutoka nyumba ya vipaji a.k.a THT akiimba jukwaani huku akionesha umahiri wake wa kukata mauno.
PICHA ZAIDI LIVE INGIA MICHUZIJR.BLOGSPOT.COM
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...