Bw Sixmund J. Begashe akila Yamini ya kuishi na Bi Neema C. Mtobesya mbele ya Baba Askofu Stanley Hotay wa Dayosisi ya Mlima Kilimanjaro, wachungaji, wasimamizi na waumini walio udhuria ibada ya ndoa iliyo fungwa katika kanisa la Anglican Magugu Babati.
Mwl Bibi Selina Daudi akikabidhi zawadi kwa wajukuu zake Maharusi Sixmund na Neema kwenye sherehe aliyo wanaandalia baada ya ibada na kuudhuriwa na zaidi ya wageni 500.
Bw Sixmund na my Wife wake Neema wakikata keki ya Ndafu huku wakishuhudiwa na wasimamizi wao Bw na Bibi Henry Gwimo mbele ya wageni waalikwa zaidi ya 600 katika Ukumbi wa CCM Babati Mjini.
Shangwe na nderemo, zilizizima katika kanisa la Anglican Magugu baada ya Bw Sixmund J. Begashe na Bi Neema C. Mtobesya kula yamini ya kupendana milele mbele ya Baba askofu Stanley Hotay wa Dayosisi ya Mount Kilimanjaro na waumini zaidi ya 500 walio hudhuria ibada hiyo takatifu ya ndoa.
Akiwaubiria wanandoa hao na waumini hao, Baba Askofu aliwaomba watanzania kuheshimiana na kuheshimu imani ya kila mmoja kwani kwa kufanya hivyo Tanzania itarudi katika ramani ya kuwa kisiwa cha amani tofauti na ilivyo sasa.
Baada ya sherehe iliyo andaliwa na Mwl Bibi Selina Daudi (Nchimbi) Mji wa Magugu na ile ya wanakamati katika Ukumbi wa CCM Babati Mjini, wanandoa hao walitoa shukrani kwa watu wote walio waunga mkono kwa hali na mali katika kufanikisha Sakramenti hii Takatifu.
Watu zaidi ya 1000 waliudhuria katika Mnuso huo.
Safi sana man kinozi ... Umetisha mzee..
ReplyDelete