Mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar inayosimamia ofisi za Viongozi wakuu wa Kitaifa Mhe.Hamza Hassan Juma akiongea na Maofisa wa Makao Makuu ya Jeshi la Polisi wakati wa ziara ya kikazi ya kamati hiyo kutembelea Makao makuu ya Polisi jijini Dar es Salaam.Kulia ni Kamishna wa Operesheni na Mafunzo Paul Chagonja na Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai DCI Robert Manumba.
Kamishna wa Operesheni na Mafunzo wa Jeshi la Polisi Paul Chagonja akizungumza wakati wa kikao cha pamoja kati ya Maofisa wa Makao Makuu na Wajumbe wa kamati ya kudumu ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar inayosimamia ofisi za Viongozi wakuu wa Kitaifa wakati wa ziara yao Makao Makuu ya Polisi jana.Kushoto ni Mwenyekiti wa kamati hiyo Mhe Hamza Hassan Juma.
Mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar inayosimamia ofisi za Viongozi wakuu wa Kitaifa Mhe.Hamza Hassan Juma akipokelewa na Mkuu wa Utawala wa Jeshi la Polisi, Naibu Kamishna wa Polisi Thobias Andengenye Makao Makuu ya Jeshi la Polisi wakati wa ziara ya kikazi ya kamati hiyo kutembelea Makao makuu ya Polisi jijini Dar es Salaam(Picha na Frank Geofray-Jeshi la Polisi).


Frank Geofray-Jeshi la Polisi

Wajumbe wa Kamati ya kudumu ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar inayosimamia ofisi za Viongozi wakuu wa kitaifa imelipongeza Jeshi la Polisi kwa jinsi linavyotekeleza majukumu yake kwa kuwachukulia hatua wachochezi wanaotumia mgongo wa siasa au dini hapa nchini. 

Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mh. Hamza Hassan Juma aliyasema hayo jana wakati wa ziara ya kamati hiyo ilipotembelea makao makuu ya Jeshi la Polisi kwa lengo la kujifunza na kuweka mikakati ya pamoja katika kukabiliana na uhalifu pamoja na kuboresha maisha ya askari Polisi.

Alisema, Jeshi la Polisi linapaswa kutomuonea muhali mtu yeyote ama taasisi itakayotumia mwamvuli wa siasa au dini kupandikiza na kueneza chuki ndani ya jamii kitendo ambacho hupelekea uvunjifu wa amani.

Aidha, Mwenyekiti wa kamati hiyo, alishauri kuwa viwanja vyote vinavyomilikiwa na Jeshi la Polisi vipatiwe hati miliki ili kupunguza uvamizi katika maeneo na viwanja vya Polisi na endapo kuna wavamizi wowote wachuliwe hatua za haraka.

Kwa upande wake Kamishina wa operesheni na mafunzo wa Jeshi la Polisi (CP) Paul Chagonja alibainisha matishio yanayoikabili nchi kwa sasa ambayo ni misimamo mikali ya kisiasa, migogoro ya wafugaji na wakulima, biashara ya dawa za kulenya, mauaji yanayosababishwa na imani za kishirikina na watu kuwania mali pamoja na ajali za barabarani zinazosababisha vifo kutokana na waendesha pikipiki na kuongeza kuwa Jeshi la Polisi limejipanga na linaendelea na mikakati mbalimbali ya kiusalama katika kukabiliana na matishio hayo ikiwemo kupeleka askari katika tarafa ili kuimarisha ulinzi ngazi ya tarafa hadi familia.

Aidha, aliwataka wananchi kuendelea kutoa ushirikiano kwa kuwafichua wahalifu waliopo kwenye jamii kabla hawajatekeleza adhima yao ya kutenda uhalifu.

Aliongeza kuwa hivi sasa Jeshi hilo linaendelea kutekeleza program ya maboresho ili kuboresha vitendea kazi pamoja na maslahi ya askari ambapo kila askari hivi sasa pamoja na mambo mengine anapata matibabu kwa kutumia bima ya afya na zaidi ya shilingi bilioni 42 zimekopeshwa kwa askari kupitia chama cha ushirika cha kuweka na kukopa cha Jeshi la Polisi ( Ura Saccos) kwa lengo la kuboresha maisha ya askari binafsi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Kwa uzito wa suala la Amani nchini,

    PANA UMUHIMU TUKA FUNGUA GEREZA MAALUM KWA AJILI YA WAHALIFU WA NAMNA HII.

    KWA KUWA MCHOCHEZI YEYOTE WA AMANI ANAKUWA NA MSIMAMO WA ITIKADI ULIOPITILIZA HIVYO WAWE TRIED KTK MAHAKAMA TOFAUTI NAKUFUNGIWA MAGEREZA MAALUM!!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...