Waziri wa Nchi Ofisi ya WaziriMkuu Sera, Uratibu na Bunge, Mhe. William V. Lukuvi (MB)akipokea maelezo kutoka kwa Meneja Mkuu wa Kituo cha Mpanda Bw. Nahoda Khatib (wakatikati)wakati wa Ziara yake kikazi katika Mkoa wa Katavi iliyoanza jana tarehe 16 Septemba,2013. Kushoto (mwenyetai) ni Bw. C. Sadda Meneja Usafirishaji Kanda ya Tabora.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Uratibu na Bunge Mhe. William V. Lukuvi (MB) akikagua Soko la Kimatifa la Mahindi la Isunta katika Wilaya ya Nkasi akiwa kwenye mwendelezo wa ziara yake ya kutembelea sehemu za Ununuzi na Uhifadhi Mahindi nchini.
Katika ziara hiyo Waziri Lukuvi amewaagiza Wakala wa Hifadhi ya Chakula NFRA pamoja na TRL kushirikiana kwa pamoja ili kuweza kuanza kusafirisha Mahindi mapema kuelekea Shinyaga kabla ya kuanza kwa mvua ili kuweza kupunguza gharama za usafirishaji katika kipindi hicho, alisema hayo tarehe 17 Septemba, 2013.
Habari Picha na Afisa Habari Ofis ya Waziri Mkuu
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...