Waziri Mkuu Mizengo Pinda (wa pili kulia) akikata utepe leo kuashiria ufunguzi wa maonyesho ya bidhaa zinazozalishwa nchini China yanayofanyika katika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam. Maonyesho hayo ya siku nne yanalengo la kutangaza bidhaa zinazozalishwa nchini humo ili viwanda na makampuni ya nchi hiyo waweze kufanya biashara na watanzania. Kulia kwa waziri mkuu ni Waziri wa Viwanda na Biashara Dk. Abdallah Kigoda na kushoto kwake ni Balozi wa China nchini LV Youqing.
Waziri Mkuu Mizengo Pinda alijaribu jembe la kupandia nafaka wakati alipotembelea banda la kiwanda cha Qingyuan Manchu Autonomous County cha nchini China wakati wa maonyesho ya bidhaa zinazozalishwa nchini humo yanayofanyika katika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam.Wanaomtazama ni Waziri wa Viwanda na Biashara Dk. Abdallah Kigoda (kushoto) na Balozi wa China nchini LV Youqing (kulia).
Waziri Mkuu Mizengo Pinda akiangalia malighafi zinazotumiwa na kampuni ya Beijing New Building Material kutengenezea nyumba alipotembelea banda hilo leo wakati wa ufunguzi wa maonyesho ya bidhaa zinazozalishwa nchini China yanayofanyika katika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam. Wa kwanza kushoto ni Meneja Msaidizi Idara ya Biashara ya Kimataifa wa Kampuni hiyo Alec Lu na wapili kulia ni Makamu Meneja Mkuu Fred Yu.
Mfanyakazi wa kiwanda cha Changzhou Amec Group cha nchini China Yan Xing Long (kulia) akimueleza Waziri Mkuu Mizengo Pinda jinsi mashine ya kuchanganya kokoto iliyotengenezwa na kiwanda hicho inavyofanya kazi wakati wa maonyesho ya bidhaa zinazozalishwa nchini humo yanayofanyika katika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam.
Waziri Mkuu Mizengo Pinda akiangalia mfano wa nyumba zinazojengwa na kampuni ya Beijing New Building Material alipotembelea banda hilo wakati wa maonyesho ya bidhaa zinazozalishwa nchini China yanayofanyika katika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam. Wapili kulia ni Waziri wa Viwanda na Biashara Dk. Abdallah Kigoda na watatu kushoto ni Meneja Msaidizi Idara ya Biashara ya Kimataifa wa Kampuni Alec Lu.
Baadhi wa watu mbalimbali walioshiriki ufunguzi wa maonyesho ya bidhaa zinazozalishwa nchini China yanayofanyika katika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam. Maonyesho hayo ya siku nne ambayo yamefunguliwa leo yanalengo la kutangaza bidhaa zinazozalishwa nchini humo ili viwanda na makampuni ya nchi hiyo yaweze kufanya biashara na watanzania.Picha na Anna Nkinda – Maelezo
Lau kama bidhaa hizo zingekuwa ni za Tanzania na zinaonyeshwa huko China.
ReplyDeleteMdau wa kwanza unakinyongo au unatoka NCHI jirani? Kama ni kweli ww ni mtz kumbuka miaka ya nyuma? Baba tulikua wapi? Na hapa tulipo sasa,sema alihamdulilah,hapo ni SERIKALI yako au waziri mkuu aseme kuanzia leo nataka kuona NCHI NZIMA ya TANZANIA inakua na NYUMBA ZA KISASA kama hizo,hapa ninamaanisha ya kwamba SERIKALI INGIE MKATABA NA HIYO KAMPUNI,mm wala sioni kosa la hao WACHINA,hao hawajatukataza kupeleka vitu vyetu kwao toka kwenye giza nene mdau mwenye kinyongo,naitwa mdudu kakakuona nipo huku UK au UINGEREZA,salamu kwa wadau wote huko home nawapenda sn,
ReplyDeleteWachina wana vitu vizuri tu,ila ni sisi wenyewe tunawaambia washushe viwango ili tuweze kujitajirisha harakaharaka,ndio maana tunaletewa low quality products.
ReplyDeleteNi sisi wenyewe watanzania wafanya biashara ndio tunawaua ndugu zetu na kuwauzia mauzauza.
Ni maoni yangu....
Mimi ni anon wa kwanza – nachangia tena ya anon wa pili kwa madhumuni ya kuelemishana tu bila malumbano yasiyo na tija; hivyo, niruhusu nitundike yafuatayo:
ReplyDeleteSana sana, sina kinyongo hata kidogo. Sitoki NCHI ya jirani. Wewe ndie mwenye kinyongo kutokana na ku-insinuate na ku-construe NCHI ya jirani kuwa ina njama za kututakia kiama!
Mimi ni Mtanzania anayekumbuka vizuri enzi za Waziri Mkuu Rashid Mfaume Kawawa na kaulimbiu yake ya kutaka “vya usasa” mathalani, nyumba ya kisasa, mapishi ya kisasa, na kadhalika. Lakini haikutekelezwa shauri ya utegemezi (na hata wa kufikiri) kutoka nchi za nje.
Mpaka leo tunashindwa kuweka madawati au kuchimba vyoo mashuleni (kana kwamba hatujui kuyatengeneza au kuvichimba) mpaka Mjapani atoe misaada na Balozi wake aje kufungua…jamani, hata choo!
Mosi, ki-protokali, hayo maonyesho yangefunguliwa tu na Balozi wa Uchina aliyeko Dar es Salaam na kuwakaribisha wenyeji wake: Waziri Mkuu na Waziri wa Viwanda na Biashara.
Pili, hivi sisi tutafanya biashara gani na Wachina kulingana na hiyo picha ya jembe la kupandia nafaka? Yaani, Tanzania ya leo hautuwezi hata kidogo kuwa watukutu wa kiasi cha kugundua jembe kama hilo? Au ni kwa sababu ya kuiga na kudai eti tumeingia katika tabaka la “middle class” (watoa nguvu na akili ya kuajiriwa na kununua kutoka soko.)
Tumewasahau wakulima, wafugaji na wavuvi, ikiwa ni pamoja na waokotaji msituni (kwa mfano, Wahzabe wa asali na nyama)! Watanzania wengi si walaji wa vya kutoka supermarkets, kama Shoprite, hivi. Ni producers and consumers au prosumers – wanavizalisha na wanavila moja kwa moja! Kwa sababu ya kuwasahau, ndio maana tunahusudu hata hilo jembe la Mchina!
Tatu, hizo malighafi, zinazotumika kujengea nyumba za kisasa, hao Wachina wanazipata kutoka wapi? Nakumbuka kulikuwepo na Waswedeni wakishirikiana na Shirika la Numba la Taifa – kupitia mradi wa Timber Utilization Unit - wakitumia malighafi zetu katika kujenga nyumba za kisasa. Utaalamu huo wa “timber utilization” ulifutika kutoka katika bongo za Watanzania.
Leo tunazidi kupiga “mark time” tumesimama na kukanyaga pale pale! La sivyo, tungeweza kuuendeleza kupitia dhana ya “transfer of learning” kwa kutumia malighali za aina nyingine.
Nne, hata utaalamu wa mashini hiyo ya kuchanganya kokoto tunao. Tunaweza kuitengeneza hapa Tanzania; sio lazima utoke nchi za nje!
Tano, Wachina ni wajanja wa kupata malighafi kutoka “shamba la bibi” – watatafuta hizo malighafi na kutengeneza bidhaa za kutuuzia! Tunajenga majumba ya magorofa kwa simenti tu na mengine yanaporomoka. Wachina wanajenga magorofa yao kwa kuyahimili kwa chuma yetu na kutengeza vijiko, uma na visu, licha ya chuma ya kujengea Daraja la Kigamboni!
Sita, asante sana kwa kudai kuwa uko Uingereza. Uingereza haikuendelea kwa kuuziwa vya nje; iliendelea kwa kutengeneza vya kwao na kuuza nchi za nje, ikiwa ni pamoja na kupata malighafi kwa urahisi kutoka nje.
Fanya utafiti kidogo hapo maktabani Uingereza au waulize Waingereza waliobobea katika fani ya historia wakufundishe jinsi Uingereza ilivyoweza kujikwamua kutoka katika rindi la umaskini hadi kuwa taifa kubwa duniani. Jaribu kwa bidii kupata majibu kwa “the rise of the industrial state – why Britain was the first to industrialize.” Ukipata majibu sahihi, basi tufundishe kidogo, ewe “mdudu kakakuona”!
Saba, ukiwa huko Uingereza, nakuomba sana uwe unaangaza-angaza macho ya “kakakuona” kuangalia makala za akina Jenerali Ulimwengu, Joseph Mihangwa au Johnson Mbwambo kwenye gazeti la Raiamwema kupitia online. Kwani ni matumaini yangu kwamba unafundishika!
Mwisho, na wewe “salamu kwa wadau wote huko abroad; nawapenda sana ninyi mlioko Uingereza!
Mdau wa kwanza nimependa statement yako ya kumjuza mdau wa pili na kuidhinisha kwa kumtaka mdudu kaka kuona kuandaza macho na awe mtafiti siyo kuwa uingereza tu. Ha ha ha ha ha safi sana kwa maelezo yako 1 mpaka 7.
ReplyDeleteKwa Ujenzi Mchina hana Mpinzani duniani!
ReplyDelete