Chama Cha Mapinduzi (CCM) kinampongeza Rais
Mstaafu wa Shirikisho la Mpira nchini (TFF) Leodger Tenga kwa uongozi wa
kutilia mfano uliowezesha kuleta mapinduzi makubwa ya mifumo ya soka nchini.
Aidha CCM inamtumia salam za pongezi za
dhati Rais Mpya wa TFF, Jamal Malinzi, na Uongozi wake wote mpya wa Shirikisho
la Soka Tanzania (TFF) uliopatikana katika uchaguzi uliofanyika juzi, Oktoba
27, 2013 jijini Dar es Salaam.
Chama Cha Mapinduzi, kinaimani kubwa na Malinzi wa wenzake katika kuendeleza jitihada zilizoanzishwa na uongozi uliomaliza muda wake sanjari na kuibua mbinu mpya zitakazoboresha na kuleta mapinduzi makubwa ya soka nchini.
Chama Cha Mapinduzi, kinaimani kubwa na Malinzi wa wenzake katika kuendeleza jitihada zilizoanzishwa na uongozi uliomaliza muda wake sanjari na kuibua mbinu mpya zitakazoboresha na kuleta mapinduzi makubwa ya soka nchini.
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Ndugu Nape
Nnauye anawaasa“Tunauomba uongozi mpya kujiepusha na jitihada za kujiendeleza binafsi
na badala yake uwekeze katika soka na kuepusha migogoro isiyo na tija katika
mchezo huo ambao kwa sasa ndio unaopendwa na Watanzania wengi”
“Daima imani huzaa imani, hivyo imani ya CCM kwako na kwa viongozi wenzako mliochaguliwa pamoja izae imani ya utumishi uliotukuka" Ndugu Nape amehitimisha.
“Daima imani huzaa imani, hivyo imani ya CCM kwako na kwa viongozi wenzako mliochaguliwa pamoja izae imani ya utumishi uliotukuka" Ndugu Nape amehitimisha.
Chama Cha Mapinduzi kinatambua kuwa migogoro
imekuwa kwa sehemu kubwa chanzo cha kukwamisha sana maendeleo ya soka hapa
nchini na hivyo kuwanyima Watanzania raha ambayo huitarajia kutoka kwenye
mchezo huo na hasa pale timu zao zinapopata ushindi.
Imetolewa na:-
Kitengo
cha Mawasiliano na Umma
Chama
Cha Mapinduzi
Ofisi
Ndogo ya Makao Makuu
Dar
es Salaam
Hongera sana malinz
ReplyDeleteHii picha ya makabidhiano baina ya outgoing president na incoming (new) president imekaa kama wako na "bifu" fulani hivi.....mbona hawatazamani usoni? - ni mtazamo tu; ila kama kuna bifu lazima limalizwe maana wote hao ni wadau muhimu wa soka!
ReplyDeleteIkiwa uongozi mpya wa TFF unatakiwa usiwekeze kwenye maendeleo binafsi bali kwenye maendeleo ya soka....(according to Nape) then inamaana kuwa uongozi unaomaliza muda wake uliwekeza katika maendeleo binafsi? kuna ushahidi huo?
CCM WASIISHIE KUPONGEZA WAACHIE VIWANJJA MANISPAA NA HALMASHAURI VIWEZE KUBORESHWA NA MPIRA UCHEZWE BILA VIWANJA BORA KAZI BURE MAKE NI AIBU TUPUUKIINGIA MKWAKWANI SOKOINE JAMHURI ABEID ARUSHA MAJIMAJI NK UNAONA AIBU KUSEMA NI VIWANJA VYA CHAMA TAWALA MIAKA 51tunajua kuna watakaoumia kimapato lakini ni muhimu kwa maendeleo ya mpira kama kweli CCM NI WANAMICHEZO
ReplyDeleteMalizi amewafungulia watu wote kuchangia maendeleo ya soka. Saafi sana. Hii inaonyesha kuwa Malinzi angependa kuona kila anayependa kushiriki kufanikisha soka Tanzania anapewa nafasi. Busara ni muhimu. Kiongozi mzuri hana makundi na kutafuta sababu za kuwafanya wengine kuwa halamu katika kuchangia maendeleo. Kunapokuwa na makosa na uvunjifu wa sheria, bado kuna fursa kwa kiongozi mwenye uwezo na hekima kuwakwamua hao wakosaji na hatimaye kufaa kwa ajili ya kazi na maendeleo ya sekta au nchi kwa ujumla wake. Makosa yaliyo nje ya mamlaka ya kiongozi husika (mfano: rushwa) hayo yatashughulikiwa na mamlaka za juu zinazohusika. Angalizo tu ni kwamba usitumie muda mwingi kuwafurahisha wajumbe. Utendaji wako hautapimwa kwa furaha uliyowapa wajumbe wa Mkutano Mkuu. Kazi ni soka la Tanzania kuimarika na kuondoa miaya ya ujanja ujanja iliyokuwepo TFF kabla ya uongozi mpya. Mwanzo mzuri na endelea kutimiza ahadi zako kwa kufuata Katiba ya TFF.
ReplyDelete