Mwenyekiti wa chama cha waandishi wa habari mkoa wa Iringa Frank Leonard kulia akitoa msimamo wa wanahabari dhidi ya gazeti la Rai na mbunge Msigwa leo ,kushoto ni katibu mtendaji wa IPC Francis Godwin
Wanahabari Clement Sanga kushoto akiwa na mwakilishi wa New habari {2006} Ltd wachapishaji wa magazeti ya Mtanzania , Rai na Bingwa mkoa wa Iringa Mercy Mwalusamba wakati wa kikao cha cha wanahabari mkoa wa Iringa leo kujadili habari zilizoandikwa na gazeti la Rai Jumapili.
Na Francis Godwin
WANAHABARI mkoani Iringa wamekanusha vikali habari zilizoandika na gazeti la Rai toleo namba 1067 la jumapili wiki iliyopita kuwa wanahabari mjini Iringa wamehongwa fedha na viongozi wa CCM mkoa wa Iringa ili wasiandike habari ya msaidizi wa mbunge Wiliam Lukuvi Bw Thom Malenga kukamatwa kwa tuhuma za kujihusisha na ujangili.
Wahanabari hao katika kikao chao kilichofanyika leo katika ofisi za klabu ya waandishi wa habari mkoa wa Iringa (IPC) mbali ya kukanusha habari hizo kuwa zimeandikwa kwa lengo la kuchafua tasnia ya habari mkoa wa Iringa ila bado wanalitaka gazeti la Rai na mbunge wa jimbo la Iringa mjini mchungaji Peter Msigwa kuwataja waandishi waliohongwa na viongozi wa CCM mkoa wa Iringa kabla ya wanahabari hao hawajachukua hatua zaidi dhidi ya gazeti la rai pamoja na mbunge Msigwa.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...