Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiwapungia mkono  wanafuzi wa  Chuo cha  Mafunzo ya Elimu ya Ufundi  Stadi(VETA) , Lindi kabla ya kuzindua mradi wa mafunzo ya gesi na mafuta ya Petroli jana mkoani Lindi.Kulia ni  Mkurugenzi Mkuu wa VETA, Mhandisi Zebadiah  Moshi na  wa pili Kushoto  ni Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Ludovick   Mwananzila na kushoto wa kwanza ni Mkuu wa Wilaya ya Lindi, Dk. Nassoro  Hamidi.
  Mwanafunzi wa  wa  Chuo cha  Mafunzo ya  Elimu ya Ufundi  Stadi(VETA), Lindi akimwonesha    Mke wa Rais Mama Salma Kikwete  kifaa cha kukata vyuma   katika karakana ya uungaji  vyuma.
 Mwanafunzi wa  wa  Chuo cha  Mafunzo ya  Elimu ya Ufundi  Stadi (VETA), Lindi akimwonesha    Mke wa Rais Mama Salma Kikwete  kifaa cha  ufundi wa magari katika karakana ya ufundi wa magari.
  Mama Salma Kikwete , akipata maelekezo kutoka kwa mwanafunzi wa Chuo cha  Mafunzo ya Elimu ya Ufundi Stadi (VETA), Edwin  Nduguru(kushoto) jinsi deep stick inavyofanya kazi ya kupima kiwango cha oil kilichopo katika injini ya gari alipotembelea karakana ya ufundi wa magari wa chuo hicho jana. Wanaoshuhudia tukio hilo ni Mkurugenzi Mkuu wa VETA, Mhandisi Zebadiah  Moshi (kulia) , Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Ludovick   Mwananzila (katikati) na Mkuu wa Wilaya ya Lindi, Dk. Nassoro  Hamidi (kushoto).
 Mama Salma Kikwete  (aliyevaa kitenge ) akiongea jambo  na  Meneja wa  British  Gas Tanzania ambao ndiyo wafadhili  wa mradi wa mafunzo ya gesi na mafuta ya Petroli, Kate Sullam (kushoto) jana  kwenye   Chuo cha Mafunzo ya Elimu ya Ufundi  Stadi(VETA) , Lindi .Kulia ni  Mkurugenzi Mkuu wa VETA, Mhandisi Zebadiah Moshi.
  Mke wa Rais  Mama Salma Kikwete  akikata utepe  ikiwa ni ishara kuzindua mradi wa mafunzo ya gesi na mafuta ya Petroli jana  kwenye Chuo cha  Mafunzo ya Elimu ya Ufundi  Stadi(VETA)  Lindi . Kulia ni  Mkurugenzi Mkuu wa VETA,  Mhandisi Zebadiah  Moshi na Kushoto wa tatu  ni Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Ludovick   Mwananzila, kushoto ni Afisa Uhusiano wa chuo hicho Dora Tesha.
  Mama Salma Kikwete  akitoa hotuba yake kabla ya kuzindua mradi wa mafunzo ya gesi na mafuta ya Petroli jana  kwenye Chuo cha  Mafunzo ya Elimu ya Ufundi  Stadi(VETA)  Lindi . Kulia ni  Mkurugenzi Mkuu wa VETA, Mhandisi Zebadiah  Moshi na Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Ludovick   Mwananzila.
 Picha ya pamoja  na baadhi ya viongozi   na wanafunzi  wa  Chuo cha  Mafunzo ya Elimu ya Ufundi  Stadi (VETA), Lindi. Picha na Anna Nkinda-Maelezo

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Serikali iangalie wilaya ya Ruangwa(Lindi),wananchi wana shida ya maji sana huko vijijini.Nimebahatika kufika(katika mizunguko yangu binafsi) vijiji vifuatavyo-Namkonjera,Nambilanje,Nandandala,Namichiga,Nusura,Mkaranga,Likakata,Moro,Namtamba kutaja vichache.Wananchi wanahangaika sana kupata maji ya kutumia(Potable water) na wakibahatika kuyapata ni yale maji ambayo si Salama.Nimetembea vijiji vingi vya Tanzania kuna matatizo ya maji ila hili la Ruangwa limenigusa na kuniuuma sana.Serikali ichimbe visima vya kutosha ikiweekana kila kijiji visima 2-3

    David V

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...