Mfuko wa Pensheni wa LAPF, umepongezwa sio tuu kwa kutoa mafao bora kuliko mfuko wowote nchini, bali ndio mfuko unaoongoza kwa kutoa mafao bora kwa nchi zote za Jumuiya ya Afrika ya Mashariki na na kwa miaka minne mfulululizo, umekua ndio mfuko unaongoza kwa kasi ya ukuaji na utunzaji vizuri wa mahesabu yake.

Pingezi hizo zimetolewa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Mhe. Hawa Ghasia, wakati, wa ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Sita wa Wadau wa LEPF, ulianza jana katika ukumbni wa AICC, mjini Arusha.

Waziri Ghasia, alizitoa pongezi hizo huku akitoa ushuhuda wa jinsi yeye alipostaafu alipata mafao kiduchu, na kulinganisha na mafao yanayotolewa sasa, hivyo kuwataka wananchi kujiunga na LAPF ili na wao wafaidike na mafao bora.

Taarifa ya LAPF kuongoza kwa mafao bora kumetolewa baada ya kufanyika utafiti wa kina, ambapo mstaafu wa LAPF, anapata Mafao ya asilimia 67% ya mshahara wake wa mwisho ambapo mafao hayo hayakatwi kodi, hivyo baadhi ya Wastaafu kujikuta wakipata fedha nyingi kuliko hata walipokuwa kazini.

Awali, Mkurugenzi Mkuu wa LAPF, Bwana . Eliud Sanga amesema, kwa miaka minne mfulululizo, LAPF imekuwa ndio mfuko unaoongoza kwa utunzani wa mahesabu kwa viwango vya NBAA. Kwa mwaka jana, iliandikisha wanachama 17,840 na umekusanya michango ya shilingi bilioni 119.7 na kwa mwaka huu unatarajia kukusanya shilingi bilioni 163.

Bwana Sanga ameeleza kuwa LAPF inaendelea kuongeza uwekezaji vitega uchumi kwa kuwekeza shilingi bilioni 570 ambapo imevuna faida ya bilioni 48.7.

Akichangia katika mkutano huo, Waziri wa Kazi na Ajira, Mhe. Gaudensia Kabaka, ameitaka mifuko ya pensheni nchini kushindana katika utoaji wa mafao bora ili wanachama wa mifuko hii wafaidike na mafao bora.

Mkurugenzi wa Mamlaka ya Usimamizi Mifuko ya Hifadhi za Jamii, Irene Isaka, amewataka wananchi kuijiunga na uchangiaji wa hiari katika mifuko mingi kadri ya uwezo wao ili utakafika umri wa kustaafu, kujikuta ndio unapata mafao bora kuliko hata mshahara wakati wa ajira.

Mkutano huo unashirikisha wajumbe zaidi ya 400 toka ndani na nje ya nchi.
 Mgeni rasmi, Waziri Ghasia, akitoa Zawadi kwa mbunge wa Arusha Mjini Mhe Goodbless Mrema ambaye ni mmoja wa wadau waliotunukiwa zaswadi kwa kuthamini michango yao mbalimbali

 MwenyeKiti  wa Bodi ya LAPF Prof. Hasa Mlawa akikabidhi zawadi Kwa Mgeni Rasmi
 Mgeni Rasmi akifurahia zawadi

.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...