Makamu wa Raisi Mh Dk Mohamed Gharib Bilal ambae pia alikua Mgeni rasmi katika Hafla ya Usiku wa Chakula cha Hisani ulioandaliwa na AMREF Tanzania kwa kushirikiana na Montage Limited na Benki M akipokea mfano wa Hundi yenye Thamani ya Shilingi Milioni 25 za Kitanzania kutoka Kwa Mwakilishi wa Benki ya NBC kwaajili ya MChango wao katika Kampeni ya Stand up For Tanzania Mother ambayo inalengo la kukusanya pesa kwaajili ya Kusomesha wakunga ili kusaidia kupunguza Vifo vya Mama na Mtoto
Mgeni Rasmi Ambaye pia Ni Makamu wa Raisi Wa Tanzania Mh Dk Mohamedi Gharib Bilal akitoa Vyeti vya kushukuru kwa wawakilishi wa Makampuni yaliyoweza kudhamini usiku huo wa Chakula cha Hisani ulioandaliwa na AMREF Tanzania kwa kushirikiana na Montage Limited na Benki M hafla iliyofanyika jana Usiku katika Hotel ya Serena
Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Montage Limited Bi Teddy Mapunda akitoa shukrani kwa Wadhamini na wahisani waliojitokeza katika Kushiriki nae kuandaa Hafla ya Usiku wa Chakula cha Hisani uliofanyika Jana katika Hotel Ya Serena ikiwa na Lengo na kutafuta pesa kwaajili ya Kusomesha Wakunga ili kuweza kusaidia katika kupata wakunga ambao Watatoa huduma na kupunga Vifo vya Mama na Mtoto hafla hiyo iliyoandaliwa na AMREF Tanzania kwa kushirikiana na Montage Limited na Bank kupitia Kampeni ya AMREF iitwayo Stand Up for Tanzania Mother iliyozinduliwa mnamo tarehe 15 Mei 2013.
Mwenyekiti wa Benki M ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Musoma Mh Nimrodi Mkono Akitoa neno kwa wageni waalikwa katika Hafla ya Usiku wa Chakula cha Hisani kwaajili ya kuchangisha pesa ya kusomesha wakunga, Hafla iliyofanyika katika Hoteli ya Serena Jana Usiku Huku ikiwa imeandaliwa na AMREF Tanzania kwa kushirikiana na Montage na Benki M kupitia Kampeni ijulikanayo Stand Up for Tanzania Mothers
Mmoja wa Wanafunzi wa Masomo ya Ukunga Kutoka Katika Jamii ya Wafugaji kutoka Kilindi Bi Tanioi Moringe Akitoa shukrani zake za dhati Kwa AMREF Tanzania ambao ndio Wameweza kumdhamini Kumsomesha Katika Chuo Cha Ukunga.
BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI
BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...