Mkurugenzi wa Huduma kwa Wanachama wa LAPF, Valerian Mablangeti, akizungumza na waandishi wa Habari kuhusu Mkutano wa Sita wa Wadau wa LAPF utakaofanyika Arusha siku ya Ijumaa na Jumamosi. Kushoto ni
Meneja wa LAPF, Kanda ya Mashariki, Amina Kassim na Kulia ni Meneja Matekelezo wa LAPF, Victor Kikoti.
Mkutano ukiendelea
Wanahabari wa Arusha wakiwa makini kazini
Mtayarishaji mashuhuri wa vipindi vya kimaendeleo katika Luninga Bw. Pascal Mayala akiwahoji viongozi wa LAPF katika mkutano huo
-------------------------------------------
Mfuko wa Pensheni wa LAPF unatarajia
kufanya mkutano mkuu wa sita wa Wadau wake tarehe 11- 12 Oktoba 2013 katika
ukumbi wa kimataifa wa mikutano wa AICC Jijini Arusha.
Kauli mbiu ya mkutano
huoni “ KUKIDHI KWA MAFAO YA KUSTAAFU;
CHANGAMOTO NA NJIA ZA KUBORESHA.” Kauli mbiu hii imefikiwa baada ya kuwepo kwa
hoja zinazojadiliwa mara kadhaa kwamba mafao ya pensheni yanayolipwa kwa wastaafu
hayakidhi. Wadau wa mkutano huu watajadili kwa kina juu ya Kauli mbiu hii na
kuona kama je ni kweli mafao
yanayotolewa yanakidhi changamoto za uzee ama ni kutokana na maandalizi
hafifu ya kustaafu.
Mkutano huu utafunguliwa na
Waziri wa nchi katika ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za
Mitaa Mhe: Hawa Ghasia
Washiriki wa mkutano huu ni
pamoja na Mamlaka ya Hifadhi ya Jamii, Waajiri wachangiaji, wanachama, vyama
vya wafanyakazi, taasisi mbalimbai za umma na binafsi pamoja na Mifuko ya
Hifadhi ya Jamii ya ndani na nje ya nchi.
Waajiri wachangiaji wa LAPF
kwa sasa wanatoka katika makundi yafuatayo:-
·
Halmashauri
zote za majiji,Manispaa, miji na wilaya nchini.
·
Wizara
zote za serikali
·
Taasisi
zote za serikali
·
Mashirika
ya umma
·
Sekta
binafsi
·
Mashirika
yasiyokuwa ya serikali (NGO’s), Wajasiriamali.
Mada mbalimbali
zitawasilishwa kutoka ndani na nje ya Tanzania zikijadili kauli mbiu hyo ambazo
ni pamoja na:
·
Mada
anzilishi juu ya kauli mbiu ya mkutano.
·
Mada
juu ya dhana ya kukidhi kwa mafao ya kustaafu.
·
Mada
ya ulinganifu wa mafao kwa nchi mbalimbali za Afrika mashariki na kati.
·
Mada
ya ujasiriamali.
·
Mada
juu ya taarifa za utendaji wa Mfuko kwa mwaka wa fedha ulioshia Juni 2013 pia zitajadiliwa
LAPF imekuwa ikifanya
mikutano hii Kubadilishana mawazo na wadau wake na kupata maoni mbali mbali
jinsi ya kuroresha huduma zinazotolewa kwa manufaa ya wanachama wake.
Kwa sasa Mfuko unatoa mafao mbalimbali kama :
·
Mafao
ya uzeeni (old age pension benefit)
·
Mafao
ya Mirathi ( survivorship benefit)
·
Mafao
ya Kuumia kazini (invalidity benefit)
·
Mafao
ya kujitoa (withdrawal benefit)
·
Mafao
ya uzazi (maternity benefits)
·
Msaada
wa mazishi (Funeral grants)
·
Mikopo
ya nyumba (House loans)
·
Mikopo
ya wanachama kupitia SACCOS
Waalikwa wote mnaombwa
kuhudhuria bila kukosa katika mkutano huu muhimu.
STAAFU KWA UFAHARI NA LAPF.
Imetolewa na Mkurugenzi Mkuu
wa LAPF.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...