Mkurugenzi wa taasisi isiyo ya kiserikali inayojishughulisha na Kilimo (ANSAF) Bw. Audax Rukonge (wa tatu kutoka kushoto) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu mkutano wa kujadili uwekezaji wa sekta ya korosho hapa Tanzania unaotarajiwa kufanyika kwa siku mbili kuanzia tarehe 4 na 5 Novemba, 2013 katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam. ANSAF kushirikiana na Bodi ya Korosho Tanzania pamoja na Baraza la Kilimo Tanzania wanaandaa mkutano utakaowakutanisha wadau na wawekezaji kutoka sekta mbalimbali kujadili na kutengeneza mipango imara itakayowezesha uwekezaji katika zao la krorsho hapa Tanzania.
Meneja Mkuu wa HANSA Group Tanzania, Bw. Vikram Verma akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya udhamini wa HANSA Group katika mkutano wa uwekezaji katika sekta ya korosho unaotarajiwa kufanyika kwa siku mbili katika ukumbi wa mikutano wa kimtaifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam. Hansa Group (Diamond Motors) ndio kampuni kutoka sekta ya usafirishaji hapa nchini inayojitolea kuisadia sekta ya kilimo hapa Tanzania kwa kutoa bidhaa bora za usafirishaji kukidhi haja ya mazingira ya Tanzania, imedhamini mkutano huu ikiamini kwamba maendeleo ya kilimo yanatokana na wadau kutoka sekta zote kukaa pamoja na kujadili njia muwafiki na mafanikio.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Mmmh hivi imani yetu itarudi kweli kwenye kilimo cha korosho?
    maana serikali ilishatutenga na kuwaacha maskini wakazi wa kusini huku wenzetu wakineemeka.
    Haya tuombe yafanikiwe nasi tupeleke wana shule.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...