Pichani kati ni Marehemu Julius Nyaisanga akiwa na wadau enzi za uhai wake,pichani kulia ni Othman Michuzi na shoto ni Aboubakar Liongo
Mtangazaji mkongwe hapa nchini,aliyekuwa Meneja Mkuu wa Kampuni ya Aboud Media, Julius Nyaisanga (Unle J), amefariki dunia leo majira ya saa moja asubuhi katika hospitali ya Mazimbu Mkoani Morogoro.
Taarifa za awali zinasema kuwa marehemu Nyaisanga alikuwa anasumbuliwa na tatizo la shinikizo la damu pamoja na kisukari.
Wakati wa uhai wake, marehemu Julius Nyaisanga alikuwa mmoja wa viongozi waanzilishi wa Kituo cha Radio One, akitokea Radio Tanzania (RTD) yeye pamoja na Mikidadi Mahmoud mwanzoni mwa miaka ya 90.
Waanzilishi wengine ni Aboubakary Liongo, Rankim Ramadhan, Flora Nducha,Vicky Msina,Taji Liundi na Blandina Munghezi.
Nyaisanga atakumbukwa sana kwa uwezo wake mkubwa wa kusoma Habari pamoja na vipindi vya muziki.Matamshi yake laini na ufasaha mkubwa wa lugha ya Kiswahili, vilimtofautisha kabisa na watangazaji wengine.
Waanzilishi wengine ni Aboubakary Liongo, Rankim Ramadhan, Flora Nducha,Vicky Msina,Taji Liundi na Blandina Munghezi.
Nyaisanga atakumbukwa sana kwa uwezo wake mkubwa wa kusoma Habari pamoja na vipindi vya muziki.Matamshi yake laini na ufasaha mkubwa wa lugha ya Kiswahili, vilimtofautisha kabisa na watangazaji wengine.
Mungu ailaze roho ya Marehemu mahali pema peponi.
RIP UNCLE J, TUTAIKUKMBUKA SAUTI YAKO YA KUVUTIA NA MBWEMBWE. POLE KWA FAMILIA NA WENGINEO WALIOGUSWA NA KUONDOKA KWAKO.
ReplyDeleteNAKUMBUKA ENZI ZAKO UPO RTD... ENZI HIZO NIPO PRIMARY SCHOOL LATE 1980S NA HATA MWANZONI MWA RADIO ONE MWANZONI MWA MMIAKA 1990S.
NAKUMBUKA MSEMO WAKO WA "PATASHIKA NGUO KUCHANIKA, SOKSI KUTOKA NA KIATU KUBAKIA"- HAHAHA!!! ULITUFURAHISHA, KUTUJUZA NA KUTUBURUDISHA UNCLE J.
FROM NAIROBI
RIP Uncle J.
ReplyDeleteTulikupenda lakini Bwana amekupenda Zaidi.
Pumzika Kwa Amani uncle.
RIP Uncle J
ReplyDeleteTulikupenda sana lakini Bwana amekupenda Saudi.
Pumzika kwa amani Uncle
sisi ni wa Allah na kwake tutarejea.katangulia nasi tujiandae.tupo ktk foleni,zamu zetu bila shaka yoyote zitafika
ReplyDeleteoooh RIP acle J Nyaisanga namkumbuka kama ancle J
ReplyDeleteWaanzilishi wa radio One umemsahau jembe Charles Hillary "mzee wa macharanga".....RIP Uncle J.
ReplyDeletemdau wa Oxford.
Sauti Yako uncle J .we will miss you
ReplyDeleteWe will miss you "Uncle J". Your voice was unique.
ReplyDeleteMwenyeez Mungu akusamehe kwa yote na akulaze pema peponi Uncle J. ( Julius Nyaisanga ) - AMEEN. Kifo ni khatma ya kila kiumbe kilichoumbwa na Mwenyeez Mungu, umetangulia nasi tupo nyuma yako. Poleni sana ndugu, jamaa na marafiki wote mliofikwa na msiba huu. Mola awajaaliye subira na stahamala katika kipindi hiki kigumu cha kuondokewa na mpendwa wetu Uncle J. - Julius Nyaisanga. Poleni sana.
ReplyDeleteRIP Uncle J
ReplyDelete