Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Auction Mart, Alex Msama (kulia), akikabidhi msaada wa thamani za ofisi kwa Rais wa Shirikisho la Filamu Tanzania (TAFF), Simon Mwakifamba (kushoto). Msaada huo wenye thamani ya milioni nne na laki tano, jijini Dar es Salaam.

MKURUGENZI wa Msama Auction Mart, Alex Msama ametoa wito kwa vijana kujikita kwenye filamu na muziki kwa sababu ndio eneo ambalo linatoa kipato halali.

Nyanja ya sanaa kwa vijana ndio eneo linaingiza pesa nyingi na kuongeza ajira kwao. Akizungumza hivi karibuni katika hafla ya kukabidhi samani za ofisi ya Shirikisho la Filamu Tanzania (TAFF) zenye thamani ya shilingi milioni 4.5, Msama alisema haoni sababu kwa vijana kujiingiza kwenye mazingira hatarishi na korofi.

Msama alisema vijana wanatakiwa wajihusishe na filamu na muziki kwa sababu ndio eneo ambalo wanaweza kutenda maendeleo yao kupitia fani hizo. “Mimi naguswa kwa kiasi kikubwa na vijana ndio maana nahangaika kusaka ufumbuzi kwao kwa kuwazuia wanaowaibia kazi zao, hii ni mojawapo ya eneo ambalo linanigusa,” alisema Msama.

Aidha Msama alisema hiyo ni mojawapo ya mikakati ya kuwasaidia vijana ili wajipatie vipato vyao. Msama ambaye pia ni Mjumbe wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) alitumia fursa hiyo kuwaeleza vijana kujitambua kwamba wao ndio nguvu kazi ya Taifa.

“Nilishangazwa na Shirikisho kama TAFF kutokuwa na ofisi, wasijione wanyonge ntaendelea kuwaunga mkono kwa kuwa kazi ya Msama Auctions Mart sio tu kukamata wezi wa kazi za wasanii pia nitahakikisha shirikisho linapiga hatua hadi mikoani,” alisema Msama.

Rais wa TAFF, Simon Mwakifwamba alimpongeza Msama na kusema kwamba ameonesha moyo wa uongozi na ulezi, Msama ni mlezi wa TAFF na kueleza kwamba serikali haijakosea kumteua kuwa mjumbe wa BASATA.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...