Kwa mara ya kwanza Siku ya ya Baba wa Taifa la Tanzania, Hayati
Mwalimu Julius Kambarage Nyerere itaadhimishwa makao makuu ya Umoja wa
Mataifa tarehe 14 mwezi huu.
Shughuli hii imeandaliwa na ubalozi wa
Tanzania katika Umoja wa Mataifa ambapo mwandishi wa idhaa ya
Kiswahili ya radio ya Umoja wa Mataifa Joseph Msami (kulia), amefanya
mahojiano na Mwakilishi wa Tanzania wake wa kudumu katika Umoja wa Mataifa Balozi
Tuvako Manongi na ameanza kwa kumuuliza ninini umuhimu wa siku hiyo?
(Mahojianao na Balozi Manongi)
Shughuli hiyo itaenda sambamba na uzinduzi wa kitabu kiitwacho JULIUS
NYERERE: Jabali wa Afrika katika medani za kimataifa kilichohaririwa
kwa pamoja na Profesa Ali Mazrui na Dokta Linda Mhando. Hayati Mwalimu
Nyerere alifariki dunia tarehe 14 Oktoba mwaka 1999 nchini Uingereza
kutokana na ugonjwa wa saratani ya damu.
First at the UN kusherehekea Mwalimu! Bravo Tanzania. Keep it up!
ReplyDelete