Profesa Paul Collier wa Chuo Kikuu cha Oxford cha Uingereza ametembelea Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Washington DC kumsalimia Mhe. Balozi Liberata Mulamula na kisha kufanya mazungumzo na Mhe.William Mgimwa,Waziri wa Fedha na Uchumi wa Tanzania katika Makao Makuu ya Benki ya Dunia,Washington DC. Mazungumzo kati ya Mhe. Waziri Mgimwa na Prof. Collier yalilenga katika kuelezea namna bora ambayo Tanzania inaweza kufaidika na rasilimali zake asilia hasa gesi kwa kutumia utaratibu wa kitaalamu na kukuza uchumi wake.
Pichani Mhe. Balozi Mulamula akiwa katika picha picha ya pamoja na Profesa Collier (kulia) na timu yake alipotembela Ubalozi wa Tanzania Washington DC.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...