Waziri Mkuu,Mizengo Pinda
WAZIRI MKUU Mizengo Pinda ameagiza iundwe tume ya kuchunguza tuhuma za ubadhirifu kwenye mradi wa maji wa Nyumbigwa wilayani Kasulu mkoani Kigoma na kutaka apewe taarifa yake katika muda wa wiki mbili.
Ametoa agizo hilo leo mchana (Ijumaa, Oktoba 4, 2013) wakati akizungumza na mamia ya wakazi wa kijiji cha Nyumbigwa kwenye uwanja wa michezo mara baada ya kuweka jiwe la msingi kwenye mradi huo wa maji.
Waziri Mkuu ambaye yuko katika siku ya nne ya ziara yake mkoani Kigoma, alimtaka Waziri wa Nchi (OWM-TAMISEMI), Bibi Hawa Ghasia aunde timu maalumu itakayoshirikisha uongozi wa mkoa, wilaya ya Kasulu na kijiji cha Nyumbigwa na kufuatilia tuhuma hizo ambazo zimetolewa na Mbunge wa Kasulu Mjini (NCCR-Mageuzi), Bw. Moses Machali.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...