KLABU ya Simba leo imeendelea kung’ang’ania kileleni baada ya kuitandika Tanzania Prisons bapo 1-0 katika mchezo uliochezwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Wakati Simba ikikaa kileleni baada ya kujikusanyia pointi 18,  watani wao Yanga nao wamezidi kuwakalia kooni baada ya kuinyuka Kagera Sugar wakiwa uwanja wa nyumbani mabao 2-1.
Yanga baada  ya ushindi huo wamerudi katika nafasi yao ya pili baada ya kufikisha pointi 15  hivyo mchezo wa watani hapo wa jadi wa Oktoba 20 ndiyo utakaoamua nani atakaa kileleni au kumfikia mwenzake.
Bao pekee la Simba lilifungwa na Jonas Mkude kwa shuti la mbali nje ya eneo la hatari na kumshinda mlinda mlango wa Prisons Beno David na mpira kukwama wavuni.
Mabao ya Yanga katika mchezo huo yalifungwa na Mrisho Ngassa na Hamis Kiiza wakati bao la Kagera lilikwamishwa wavuni na Godfrey Wambura.
Mchezo mwingine wa Ligi hiyo uliochezwa kwenye Uwanja wa Chamanzi Ashanti United walizinduka na kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Coastal Union.
Dakika ya 2 Mpira ulirushwa kama kona na Kipa wa Kagera Sugar kuupangulia kwa Mshambuliaji wa Yanga Mrisho Ngassa ambaye alifanikiwa kuipatia bao na hapa walikuwa wanashangilia bao hilo. Mpaka Mapunziko Yanga ilikuwa inaongoza kwa bao 1-0 dhidi ya Wenyeji Kagera Sugar.

Wachezaji wa Yanga wakishangilia Baada ya kupata bao kupitia kwa Mrisho Ngassa. Kwa Picha zaidi toka Bukoba BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...