Wahamiaji haramu 16 kutoka nchini somalia wamekamatwa Mkoani morogoro
wakiwa wamejificha katika lori la mizigo lililosheni chokaa
likitokea jijini dar es salaam kuelekea mkoani mbeya
Kupatikana kwa wahamiaji haramu hao kunatokana na ushirikiano wa
wananchi ambao umesaidia kukamatwa kwa wahamiaji hao huku wakidai kuwa
baadhi yao walikosa hewa kufuatia kujificha katika mizigo hiyo
Kwa upande wake afisa
uhamiaji mkoa wa Morogoro Hamprey Minja amesema kuwa dereva wa gari hilo
amekamatwa na kufikishwa kituo cha polisi ambapo amesema kuwa vyombo vya
ulinzi na usalama vimedhibiti kwa kiasi kikubwa maeneo ya mipaka kwa ajili ya
kudhibiti matukio ya wahamiaji haramu hali inayopelekea wahamiaji hao kutumia
njia nyingine ikiwemo ya kujificha katika magari ya mizigo.
Hao madereva wafungwe miaka mingi kwa kubeba raia sehemu ya mizigo na kusababisha vifu vyao...lst time walikufa watu kutoka ethiopia na sasa somalia....inaonekana huyo jamaa hafanani na msomali..lakini wachukuliwe hatua kali sana...wakimbizi warudishwe kwao sio kuwafunga
ReplyDeleteHuyo dereva na vinara Wa huo mtandao wanastahili kunyongwa. Kuwakaribisha wasomali tena wahamiaji haramu wakati huu ambao hata hatujapona majeraha ya westgate mall ni kuliangamiza taifa letu.
ReplyDelete