Sehemu ya dawa zilizokamatwa katka Operesheni.

Mkurugenzi MKuu wa TFDA na DCI Manumba wakitazama sehemu ya dawa zilizokamatwa.

Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA ) imekamata dawa bandia zenye thamani ya TSh. 49,634,733/= katika operesheni maalum ijulikanayo kama Operesheni GIBOIA iliyoshirikisha Jeshi la Polisi nchini, Shirikisho la Polisi la Kimataifa (Interpol), Baraza la Famasi, TAMISEMI, Bohari ya Dawa (MSD), Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Shirika la Viwango (TBS), Tume ya Ushindani  (FCC), Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Ofisi ya Mwendesha Mashtaka wa Serikali  (DPP), Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa  (TAKUKURU), Ofisi ya Rais na Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii.  

Operesheni GIBOIA ilifanyika kuanzia tarehe 1-3 Oktoba, 2013 katika mikoa tisa ya Tanzania Bara ambayo ni Mwanza,  Shinyanga, Mara,  Geita,  Mbeya,  Arusha,  Kilimanjaro,  Dodoma  na Dar es Salaam. Operesheni hii pia imefanyika sanjari katika nchi saba zilizopo Kusini mwa Jangwa la Sahara ambazo ni Afrika ya Kusini, Angola, Malawi, Msumbiji, Swaziland, Zambia na Tanzania kwa lengo la kupambana na dawa Bandia Barani Afrika.

Wadau wa habari wakifuatilia maelezo kuhusu Operesheni GIBOIA.

Mkurugenzi wa makosa ya jinai nchini Kamishna Robert Manumba na Mkurugenzi Mkuu wa TFDA katika mkutano na waandishi aw habari.

Mkurugenzi Mkuu wa TFDA, Hiiti Sillo akieleza waandishi kuhusu Operesheni GIBOIA.

Sehemu ya wadau wa Operesheni GIBOIA ktk mkutano.

DCI Manumba akitoa matokeo ya Operesheni GIBOIA kwa waandishi wa habari.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. Dawa bandia zitatuua. Nilimeza panadol, tumbo likauma wiki nzima kama mtu aliekula sumu vile.

    Watanzania jamani msipende sana pesa, mjali afya za watu

    ReplyDelete
  2. Hao waliokamatwa nazo kwanini wasinyongwe ili iwe fundisho kwa wengine jamani,,coz hao ni wauwaji wakubwa wa jamii yetu ya KITANZANIA,,Hongera sn KIKWETE kwa hii MISAKO tunaona sasa MATUNDA YAKE.

    ReplyDelete
  3. Duu mpaka KY nazo feki?

    ReplyDelete
  4. watu wenyewe tupo wachache bado mnataka kutumaliza, mnataka muishi peke yenu

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...