Kutokana na vipigo vya mfululizo kutoka kwa wapinzani wetu wakiwepo Pugu Veterans, na tambo nyingi kutoka kwa wapinzani wetu hapa jijini, Golden bush tumelazimika kuomba mechi ya kirafiki ya marudiano na Pugu Veterans, game itapigwa uwanja wa Kinesi maarufu kama St James Park siku ya jumapili asubuhi. 

 Kwakutambua umuhimu ya game hii, uongozi wetu umeitisha kikao cha dharula kesho baada ya mazoezi asubuhi ili kuweka mikakati kabambe ya kurudisha heshima ya timu yetu ambayo mpaka sasa inatambulika kama mabingwa wa jiji la Dar es Salaam. 

Timu yetu imekamilika kabisa hakuna majeruhi hakuna mgonjwa hakuna mgogoro, uwanja uko sawa kamati ya ufundi inamaalizia kazi yake kwa kushirikiana na Walimu wetu. Tumejiwekea lengo la kufunga magoli mengi iwezekanavyo ili kuvunja rekodi ya kufunga magoli.

Aidha ningependa kutoa taarifa kwamba timu yetu imeimarika zaidi  mara baada ya Juma Kaseja, Said Swedi ,Mwarami Mohamed na Shadrack Nsajigwa  kurejea kwenye timu yetu.  karibuni mje muone soka la hali ya juu sana huku likihanikizwa na ufundi wa vijana wa zamani chini ya kocha wetu Madaraka Selemani “Mzee wa kiminyio”

Baada ya game ya jumapili, timu itakuwa kwenye maandalizi ya mwisho kabisa kwenda kucheza mechi za kirafiki visiwani Zanzibar.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Asee jombaa njooeni Arusha chalii yangu kuna chama la wazee linaitwaga KITAMBI NOMA! ni shidaa!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...