Waziri wa Ujenzi Dkt. John Pombe Magufuli amesema kuwa Serikali imeweza kuokoa kiasi cha Shilingi bilioni 18 kwa kutumia makandarasi wa kizalendo kujenga Daraja la Mbutu. Akiwa katika ziara ya kukagua maendeleo ya mradi huo, Waziri Magufuli amebainisha kuwa ujenzi wa daraja hilo umegharimu kiasi cha Shilingi bilioni 12 badala ya Shilingi bilioni 30 endapo lingejengwa na Makandarasi wa nje.

Daraja la Mbutu pamoja na tuta la barabara lenye urefu wa kilometa 3 linajengwa na muungano wa Makandarasi wa Kizalendo 13 unaojulikana kama Mbutu Bridge Joint Venture chini ya usimamizi wa muungano wa Wahandisi Washauri wawili (2) unaojulikana kama PIDAEL Joint Venture. Makandarasi hao wanafanyakazi ya kusanifu na kujenga kwa wakati mmoja kwa gharama hiyo ya Shilingi bilioni 12 ambapo fedha zote zimetolewa na Serikali ya Tanzani.

Mkataba wa ujenzi wa Daraja la Mbutu ulisainiwa Aprili, 2012 na umepangwa kukamilika mwishoni mwa mwaka huu wa 2013.

“Nimeridhishawa na kasi ya ujenzi wa daraja hili na nimeona tayari mmefikia karibu asilimia 80, hii ni kazi nzuri inayostahili kupongezwa kwani mmeanza kudhihirisha uwezo wenu kama Makandarasi wazalendo” alisisitiza Waziri Magufuli na kuwataka Makandarasi hao kuhakikisha kuwa wanaukamilisha mradi huo kwa muda na viwango vilivyopangwa.

Mheshimiwa Magufuli pia amewataka wananchi wa maeneo hayo kuhakikisha kwamba wanalitumia daraja hilo vizuri kwani hiyo ni fursa nyingine ya kuwaletea maendeleo. Hata hivyo aliwatahadharisha wasafirishaji watakaotumia daraja hilo kuzingatia sheria za usalama barabarani kwa kutozidisha uzito uliowekwa kisheria.

Mkuu wa Wilaya ya Igunga Bw. Elibariki Kingu, kwa upande wake alimshukuru Waziri Magufuli na kwamba mambo aliyojionea na kutoa maelekezo yatasaidia kukamilika kwa daraja hili kwa wakati na hivyo kuleta faraja kubwa kwa wananchi wengi wanaoitumia barabara hiyo.

Katika hatua nyingine, Waziri Magufuli amewahakikishia wananchi wa Igunga kuwa Serikali itajenga barabara ya lami kutoka mji wa Igunga hadi Mbutu. Azma hiyo imetokana na maombi ya wananchi wa maeneo hayo waliyoyatoa katika nyakati tofauti na pia kwa kuzingatia adha iliyokuwa ikiwakabili kiasi cha kufikia baadhi ya wananchi na mifugo yao kupoteza maisha kutokana na kutokuwepo kwa mawasiliano ya barabara na daraja la uhakika katika eneo hilo hasa nyakati za mvua.
Waziri wa Ujenzi Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli (kushoto) akiwa na Mkuu wa Wilaya ya Igunga Bw. Elibariki Kingu (kulia), wakikagua maendeleo ya ujenzi wa Daraja la Mbutu linalojengwa katika wilaya ya Igunga mkoani wa Tabora.
Waziri wa Ujenzi Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli (mbele) akikagua maendeleo ya ujenzi wa Daraja la Mbutu linalojengwa katika wilaya ya Igunga mkoani wa Tabora.
Waziri wa Ujenzi Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli (mbele) akikagua maendeleo ya ujenzi wa Daraja la Mbutu linalojengwa katika wilaya ya Igunga mkoani wa Tabora.
Waziri wa Ujenzi Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli (mbele) akikagua maendeleo ya ujenzi wa Daraja la Mbutu linalojengwa katika wilaya ya Igunga mkoani wa Tabora.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

  1. Well done Eng. Joseph Maganga and co.

    ReplyDelete
  2. sasa mambo sii hayaa..kuita wachina waje kutuibiaa mali zetu...mpaka lini tutajikombowaaa kiakili??? ajira zenyewee hamna halafu tunazidisha idadi ya watu kutoka njee...wapeni vijana ajira

    ReplyDelete
  3. jee ubora wa hilo daraja utakuwa vipi? msiweke uzalendo mbele kuhatarisha maisha ya wananchi wapeni kazi wenye ujuzi na sifa hata kama ni wageni , tunachotaka ni daraja lenye kiwango cha kimataifa

    ReplyDelete
  4. Kweli acha siasa iitwe si hasa...
    yaani daraja linaoneka hata asilimia hamsini bado,wanatwambia limefikia 80!
    Hata hivyo hapo hakuna cha kuokoa maana bila shaka tenda zilitangazwa na hao jamaa ndo walishinda tenda..sasa wameokoa nini!

    ReplyDelete
  5. Blog ya jamii naomba nafasi kidogo hapa niongelee hili sakata la wenye Malori yanayozidisha uzito(overweight).Mimi sitauma maneno wala nini Dr.Magufuli yuko sawa kwenye uamuzi wake ule ambao wenye malori wanaugomea.Juzi nilibahatika kupita hii barabara kuu ya Dar-Chalinze-Dodoma-Mwanza na gari binafsi na kujionea hali halisi ya hii barabara(Sina uhakika na barabara ya Moro-Tunduma.Sina uhakika kama tatizo ni uzito wa ziada kwenye malori au ubora wa barabara zenyewe lakini barabara inaharibika sehemu nyingi(inabonyea,inabomoka).Na sehemu nyingi nimeona serikali(ya CCM!) inahangaika kuikarabati upya(inasikitisha),wizara imeweka matangazo kibao barabarani kuwaelimisha waTZ kutunza hizi barabara.WM asiwachekee hawa waharibifu wa barabara.Hongera Dr.Magufuli

    David V

    ReplyDelete
  6. We mdau unayesema daraja liwe na hadhi ya kimataifa don`t worry, PIDAEL ni kibogo kwa madaraja, wala usiwe na noma,na wee unajua madaraja kusema ati ni 50%, serikali, acha wivu wa kimaendeleo, kama waziri amerithika na kazi, mayowe yako yataishis kwenye kolomelo lako.

    ReplyDelete
  7. Tuwezeshe wazawa kwa kuwapa kandarasi ili kupunguza gharama, kuongeza ajira, na mapato kwa raia na pesa zibaki hapa hapa. Makandarasi wana wajibu kuboresha utenda kazi wao kwa kiwango cha juu. Kenya imepitisha sera ya kutoa asilimia 30 ya zabuni za serikali kwa vijana wanawake na walemavu ambao wataanzisha makampuni yanayoeleweka.

    ReplyDelete
  8. Jambo usilolijuani kama usiku wa giza....onamtu anabisha eti darajahilo halijafika 80% kwa sababu anaona kwa macho hata deki halijafunikwa. Ndugu yangu hayo ni mambo ya ufundi fani za watu hizo. zaidi ya 80% ya kazi hiyo ipokatika hizo nguzonapiles ambazo zimesimikwa chini na hazionekani

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...