Waziri wa Katiba na Sheria Mh. Mathias Chikawe (kushoto) akisisitiza jambo kwa Mtendaji Mkuu wa RITA Bw. Philip Saliboko na Mkurugenzi Mkuu wa ofisi ya Taifa ya Takwimu Dk. Albina Chuwa (kulia) walipomtembelea ofisini kwake leo 10/10/2013 jijini Dar Es Salaam na kumueleza mkakati wa usajili wa matukio muhimu ya maisha na takwimu.
Mtendaji Mkuu wa RITA Bw. Philip Saliboko (wa kwanza kushoto), Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Dk. Albina Chuwa (wa pili kushsoto) na watendaji wengine kutoka RITA wakimsikiliza kwa makini Waziri wa Katiba na Sheria Mh. Mathias Chikawe (hayupo pichani) walipomtembelea ofisini kwake jijini Dar Es Salaam na kumueleza mkakati wa usajili wa matukio muhimu ya maisha na takwimu.
Kitambulisho cha Taifa na Leseni za kuendeshea gari(Nadhani ukiwa na leseni huitaji I.D) zinaweza kuwekewa kumbukumbu za matukio aliyofanya mwanachi muhusika kwa matumizi ya baadae,mambo ambayo yanaambatana na kumbukumbu hizo ni kama ajali za barabarani,driving violation,non-driving violation ,Driving while intoxicated (DWI)or (DUI), wizi,utapeli,domestic violence, jail record,sexual harassment,nk nk.
ReplyDeleteHii inaweza kutuongoza kuwa watiifu wa sheria na pia kuondoa baadhi ya tabia mbaya ambazo zitamkwamisha muhusika mbele ya maisha kwa kuwa zitaweka wazi tabia zake kwa waajiri au jamii.
Mdau hapo juu. Wazo zuri na hilo nadhani wahusika wangeliangalia kwani driving licence na hizo ID'S ingawa ni vitu viwili tofauti lakini lengo haswa ni kumtambulisha muhusika mahala husika kwa jambo husika.
ReplyDelete