Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dkt. Fenella Mukangara (aliyevaa nguo ya
kijani) akifungua CD kuashiria uzinduzi wa filamu ya kuelimisha jamii kuhusu umuhimu wa
ununuzi wa HISA na faida zake kwa jamii. Hafla ya uzinduzi wa filamu hiyo iliyoigizwa na
Wasanii kutoka nchi za Afrika Mashariki imefanyika leo Jijini Dar es Salaam na imeratibiwa na
Soko la Hisa la Dar es Salaam.
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dkt. Fenella Mukangara (aliyevaa nguo ya
kijani) akiwa katika picha ya pamoja na Wasanii kutoka nchi za Afrika Mashariki walioigiza
filamu ya kuhamasisha jamii kuhusu umuhimu wa kununua HISA. Wa kwanza kulia ni
Mkurugenzi Msaidizi wa Maendeleo ya Utamaduni upande Sanaa, Bibi. Leah Elias.
(Picha na Kitengo cha Mawasiriano Serikalini,
Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...