Wakazi
wa Makete mjini wilayani Makete mkoani Njombe wameonesha mfano wa
kuigwa na nchi nzima baada ya kutii agizo la serikali liliowataka
kubomboa nyumba zilizopo kandokando mwa barabara ndani ya kipindi cha
mwezi mmoja
Zoezi
hili la kubomoa nyumba hizo lilitakiwa kufanywa ndani ya kipindi cha
mwezi mmoja ili kupisha ujenzi wa barabara ya lami Makete mjini kama
ilivyoahidiwa na serikali
Mtandao
huu ulishuhudia zoezi la kubomoa nyumba hizo likitekelezwa kwa zaidi ya
asilimia 95 huku wananchi hao wakiitaka serikali kuharakisha kujenga
barabara hiyo kwa wakati kwa kuwa wameahidiwa kwa muda mrefu
"Sisi
tunapenda maendeleo ya wilaya yetu ndio maana unaona tunabomoa bila
usumbufu, lakini isiwe tunabomoa halafu ujenzi unakuja kuanza miaka
ijayo huko mbele huu utakuwa ni uonevu wa hali ya juu kwa kweli" alisema
mfanyabiashara mmoja aliyejitambulisha kwa jina moja la Chaula
Wabomoaji
hao wameendelea kubomoa nyumba zao kwa umakini na kuchukua baadhi ya
vifaa kama tofali, milango, madirisha na mbao ili waweze kwenda
kuvitumia kwenye maeneo mengine waliyoyapata
Kwa
mujibu wa tangazo la TANROADS mkoa wa Njombe, zoezi la kubomoa kwa
hiari limemalizika na kwa yeyote ambaye hatakuwa ametii amri hiyo, bomoa
bomoa ya serikali itapita ili kuondoa jengo hilo(na www.edwinmoshi.com)
Nadhani walilipwa kwa wakati muafaka na kupewa maeneo mapya kwa wakati muafaka.Iwapo maeneo yote yaliyopita na hata yaliyo ktk mipango kama hii kwa siku za usoni yatafanyiwa utaratibu huu naamini hutasikia mtu akilalama au kuleta usumbufu.Bila kusahau uongozi wa eneo husika kusimama imara kwa kuwajuza wananchi wa maeneo yao kila linaloendelea mpaka kufikia hatua ya kubomoa,vinginevyo lawama,au usumbufu hautaepukika.
ReplyDelete