Siku ya 5 ya ziara ya CHADEMA Kanda ya Magharibi imetufikisha Jimbo la Igalula, wilaya ya Uyui. Tumekutana na wananchi katika vijiji vya Goweko, Loya, Miswaki, Miyenze na Kigwa.

Tumezungumza kuhusu changamoto ya usafiri wa Reli, wafugaji kunyanyaswa na watendaji wa kata na askari kwa kunyanganywa mifugo, zao la Tumbaku, maji safi na salama na suala la jumla la Katiba na mchakato wa kuandika katiba.

Kimsingi shughuli za kiuchumi za wananchi ni kubwa na hasa Kilimo na mifugo. Hata hivyo ukosefu wa miundombinu unafanya wananchi wasipate thamani ya mazao yao na jasho la kazi zao.

Nilipofika Kijiji cha Loya nimeona eneo kubwa lina miti ya mihama. Wananchi wanatumia tu mihama wakati wa njaa na mara nyingi matunda haya yanaharibika tu. Lazima matunda haya yana matumizi yake ya kiviwanda maana ‘kernel’ yake ina mafuta.
Na hili ni swali aliloacha Mh Zitto Kabwe
Nani anajua matumizi ya Mihama?

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Mheshimiwa Kabwe
    Mahama waachie tembo, ukitaka kuwasaidia wananchi hapo, waletee miche ya michikichi kutoka Brazil au Indonesia, naona ardhi hiyo can support palm trees well.

    ReplyDelete
  2. Nyoa ndevu bwana Zitto utakuwa smart jua we ni kioo.style gani hiyo?????

    ReplyDelete
  3. kunyoa ndevu sio usmat bali ni mapendekezo ya mtu mwenyewe. sisi wengine kwetu ndevu ni ishara ya mwanaume na pambo la dume waweza eka style utakayo.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...