Dkt. Ramadhani K. Dau Mkurugenzi Mkuu wa NSSF leo amechaguliwa kuwa Mjumbe wa Bodi (Bureau) wa International Social Security Association (ISSA) yenye Makao Makuu yake Geneva Uswisi. Uchaguzi huo uliofanyika Leo Mjini Doha Qatar katika mkutano wa ISSA ambao ulihudhuriwa na watu zaidi ya 1000 Kutoka nchi 127.
Hii ni Mara ya pili kwa Dkt Dau kuchaguliwa katika Bodi hiyo baada ya kuchaguliwa mwaka 2010 katika mkutano uliofanyika Cape Town Afrika Kusini. Mkutano ujao Kama huo utafanyika Mjini Natal Brazil mwaka 2016.
Wajumbe wakiwa katika foleni ya kupiga kura
Zoezi la kura likiendelea
Meza kuu wakati wa mkutano huo
Dkt. Dau akipongezana na Rais na Mweka Hazina wa ISSA
baada ya kuchaguliwa kuiongoza ISSA kwa kipindi kingine cha miaka mitatu Leo huko Doha, Qatar
Dr Ramadhani K
Dau akiwa na Mwenyekiti wa Bodi ya NSSF Kenya Bw. Adan Mohamed leo katika
mkutano wa International Social Security Association (ISSA) uliofanyika huko Doha, Qatar
Hongera sana Dr. DAU kwa kuiwakilisha vyema Tanzania na kuiletea sifa kubwa nchi yetu katika uwanja wa kimataifa. Indeed also this is another well deserved personal achievement which of course showcases your outstanding Leadership and Commitment in your field and other areas. Well done DC.
ReplyDeleteMdau Diaspora UK.
Hongera sana Sheikh Dr. Dau!
ReplyDeleteInshallah Mwenyezi Mungu akuzidishie!!!
CONGRATS BRO, HAKUNA HAJA YA MANENO VITENDO YANAJIELEZA, ALLAH AKUWEZESHE NA MAJUKUMU
ReplyDeleteHongera sana Dr. Ramadhani Dau, Umetuwakilisha vizuri wana Diaspora
ReplyDeleteMdau, Mshike
Lewisham - UK
Hongera Dr. Hii ni Ishara tosha kuwa wewe ni JEMBE.
ReplyDeleteMdau Ramadhani Nassib (Na. 17)
Safi sana Kamanda. Wewe ni Ishara Tosha kuwa ni Kiigizo chema na kiongozi bora ndani na nje ya nchi, Hongera kwa kuchana mawimbi.
ReplyDeleteMdau Meya London/Barking
Hongera sana Dr. Ramadhani Dau.
ReplyDeleteUmetisha Mbaya
Pawassa - Buguruni
Safi sana Dr. Uwezo unao, sababu tunazo, Unakubalika sana, Tunakutakia kila la Kheri na Mungu akuongoze na kukupa nguvu zaidi.
ReplyDeleteSiki Magoha
hongera sana Dr Ramadhani Dau..kwa hilo hila punguza udini ,maana katika uongozi wako sehemu fulani ,kazi ni kwa waislam tuu .sisi wenye majina ya kigalatia hata kama cv ilikuwa imeshiba lakini hola...,Asante asiyependa UDINI
ReplyDeleteAsiyependa UDINI, inamaana Wafanyakazi wote waislamu? Hayo ni maneno ya vijiwe vya Kahawa, Jamaa ni JEMBE.
ReplyDeleteMnyonge mnyongeni na haki yake mpeni!
Hongera sana Alhaji, Dr.Dau Kazi unayoifanya haihitaji hata elimu ya form IV kuweza kukutathmini juu ya utendaji wako. Miradi yako ina faida ndani na nje ya nchi kwa mfano daraja la kigamboni. Kwa ujumla miradi yako ina tija ktk kuongeza kasi ya kukua kwa uchumi, pato la mwanachi na huduma kwa jamii.
ReplyDeleteHongera sana, Tunakuombea maisha marefu.
Msemakweli
Hongera sana alhaji, Tathmni ya utendaji wako umepimwa na wajumbe wa nchi 127. Hii ni kipimo tosha cha utendaji wako. zaidi ya hapo miradi yako ina tija kwa wananchi, taifa na mataifa mengine mfano daraja la kigamboni.
ReplyDeletehongera sana
Msemakweli
Hongera sana Dr. Dau, endelea kulitumikia Taifa letu kwa nguvu zako zote, na usikate tamaa kutokana na maneno ya wasiopenda mafanikio ya Taifa hili.
ReplyDeleteDewa - Arusha