Dkt.  Ramadhani K. Dau Mkurugenzi Mkuu wa NSSF  leo amechaguliwa kuwa Mjumbe wa Bodi (Bureau) wa International Social Security Association (ISSA) yenye Makao Makuu yake Geneva Uswisi. Uchaguzi huo uliofanyika Leo Mjini Doha Qatar katika mkutano wa ISSA ambao ulihudhuriwa na watu zaidi ya 1000 Kutoka nchi 127. 
 Hii ni Mara ya pili kwa Dkt  Dau kuchaguliwa katika Bodi hiyo baada ya kuchaguliwa mwaka 2010 katika mkutano uliofanyika Cape Town Afrika Kusini. Mkutano ujao Kama huo utafanyika Mjini Natal Brazil mwaka 2016.
Wajumbe wakiwa katika foleni ya kupiga kura
Zoezi la kura likiendelea
 Meza kuu wakati wa mkutano huo

Dkt. Dau akipongezana na Rais na Mweka Hazina wa ISSA baada ya kuchaguliwa kuiongoza ISSA kwa kipindi kingine cha miaka mitatu Leo huko Doha, Qatar
Dr Ramadhani K Dau akiwa na Mwenyekiti wa Bodi ya NSSF Kenya Bw. Adan Mohamed  leo katika mkutano wa International Social Security Association (ISSA) uliofanyika huko Doha, Qatar

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 13 mpaka sasa

  1. Hongera sana Dr. DAU kwa kuiwakilisha vyema Tanzania na kuiletea sifa kubwa nchi yetu katika uwanja wa kimataifa. Indeed also this is another well deserved personal achievement which of course showcases your outstanding Leadership and Commitment in your field and other areas. Well done DC.
    Mdau Diaspora UK.

    ReplyDelete
  2. Hongera sana Sheikh Dr. Dau!

    Inshallah Mwenyezi Mungu akuzidishie!!!

    ReplyDelete
  3. CONGRATS BRO, HAKUNA HAJA YA MANENO VITENDO YANAJIELEZA, ALLAH AKUWEZESHE NA MAJUKUMU

    ReplyDelete
  4. Hongera sana Dr. Ramadhani Dau, Umetuwakilisha vizuri wana Diaspora

    Mdau, Mshike
    Lewisham - UK

    ReplyDelete
  5. Hongera Dr. Hii ni Ishara tosha kuwa wewe ni JEMBE.

    Mdau Ramadhani Nassib (Na. 17)

    ReplyDelete
  6. Safi sana Kamanda. Wewe ni Ishara Tosha kuwa ni Kiigizo chema na kiongozi bora ndani na nje ya nchi, Hongera kwa kuchana mawimbi.

    Mdau Meya London/Barking

    ReplyDelete
  7. Hongera sana Dr. Ramadhani Dau.
    Umetisha Mbaya

    Pawassa - Buguruni

    ReplyDelete
  8. Safi sana Dr. Uwezo unao, sababu tunazo, Unakubalika sana, Tunakutakia kila la Kheri na Mungu akuongoze na kukupa nguvu zaidi.

    Siki Magoha

    ReplyDelete
  9. hongera sana Dr Ramadhani Dau..kwa hilo hila punguza udini ,maana katika uongozi wako sehemu fulani ,kazi ni kwa waislam tuu .sisi wenye majina ya kigalatia hata kama cv ilikuwa imeshiba lakini hola...,Asante asiyependa UDINI

    ReplyDelete
  10. Asiyependa UDINI, inamaana Wafanyakazi wote waislamu? Hayo ni maneno ya vijiwe vya Kahawa, Jamaa ni JEMBE.

    Mnyonge mnyongeni na haki yake mpeni!

    ReplyDelete
  11. Hongera sana Alhaji, Dr.Dau Kazi unayoifanya haihitaji hata elimu ya form IV kuweza kukutathmini juu ya utendaji wako. Miradi yako ina faida ndani na nje ya nchi kwa mfano daraja la kigamboni. Kwa ujumla miradi yako ina tija ktk kuongeza kasi ya kukua kwa uchumi, pato la mwanachi na huduma kwa jamii.

    Hongera sana, Tunakuombea maisha marefu.

    Msemakweli

    ReplyDelete
  12. Hongera sana alhaji, Tathmni ya utendaji wako umepimwa na wajumbe wa nchi 127. Hii ni kipimo tosha cha utendaji wako. zaidi ya hapo miradi yako ina tija kwa wananchi, taifa na mataifa mengine mfano daraja la kigamboni.

    hongera sana
    Msemakweli

    ReplyDelete
  13. Hongera sana Dr. Dau, endelea kulitumikia Taifa letu kwa nguvu zako zote, na usikate tamaa kutokana na maneno ya wasiopenda mafanikio ya Taifa hili.

    Dewa - Arusha

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...