Na Mwandishi Wetu
MWIMBAJI wa muziki wa Injili kutoka nchini Zambia, Ephraim Sekeleti, atatumbuiza kwenye Tamasha la Krismas litakalofanyika Tanzania mwaka huu.
Tamasha la Krismas linaandaliwa na Kampuni ya Msama Promotion ya jijini Dar es Salaam na litafanyika Desemba 25 Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na siku inayofuata Uwanja wa Jamhuri, Morogoro.
Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya tamasha hilo, Alex Msama, katika taarifa yake kwa vyombo vya habari jana, alisema tayari wameshakubaliana na msanii huyo na kwamba atapiga nyimbo zake katika albamu mbalimbali ikiwemo ile ya Mungu Mwenyewe.
Baadhi ya nyimbo maarufu za msanii huyo Uniongoze na Kidonge cha Yesu, ambazo ni kivutio kikubwa kwa mashabiki wa muziki wa kiroho hapa nchini.
“Kwanza kabisa tofauti na Tamasha la Pasaka, hili la Krismas tutakuwa na waimbaji wengi zaidi wa muziki wa Injili kutoka nchi za nje na wale wa kali wa hapa Tanzania.
“Wapendwa wajiandae kushiriki kwa wingi kwani watashiba kiroho kutokana na kuwa na waimbaji wengi wenye hamasa ya kiroho,” alisema Msama ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi Tamasha la Pasaka.
Waimbaji wengine waliothibitisha kushiriki Tamasha la Krismas mpaka sasa ni Upendo Nkone na Upendo Kilahiro ambao wote ni Watanzania na kwamba mazungumzo na wasanii wengine mahiri wa nje na ndani ya Tanzania yanaendelea.
Msama this is too much publicity.
ReplyDeleteIs this a spiritual thing or a commercial concert? It is like any other musiq concert FIESTA, KILI MUSIQ AND THE LIKE
Sasa kuna tatizo gani akifanya publicity ya tamasha la nyimbo za injili ili habari ziwafikie waumini zaidi? Mie nadhani anatakiwa kupongezwa kwa hilo...mbona hamlalamiki yakitangazwa hayo mengine? You cant be serious
ReplyDelete