Kamishna wa Sheria na Uendeshaji wa Magereza, Dkt. Juma Malewa akitia
saini kwenye Kitabu cha Wageni katika Ofisi ya Mkuu wa Gereza la Mahabusu
Morogoro baada ya kuwasili Gerezani hapo tayari kwa ziara ya kikazi akikiwa
ameongoza na Mkuu wa Magereza Mkoa wa Morogoro na Maafisa Waandamizi wa
Magereza kutoka Makao Makuu ya Jeshi la Magereza, Dar es Salaaam.
Kamishna wa Sheria na Uendeshaji wa Magereza(wa pili toka kulia)
akikagua maeneo mbalimbali ndani ya Gereza la Mahabusu Morogoro katika ziara
yake ya kikazi aliyoifanya Novemba 1, 2013(wa kwanza kulia) ni Mkuu wa Magereza
Mkoa wa Morogoro, Naibu Kamishna wa Magereza, James Selestine(kushoto) ni
Mthibiti Mkuu wa Fedha wa Jeshi la Magereza, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa
Magereza, Gideon Nkana.
Baadhi ya Maafisa wa Jeshi la Magereza wa Gereza la Mahabusu Morogoro
wakiwa timamu kwa kazi za siku hiyo wakati Kamishna wa Sheria na Uendeshaji wa
Magereza, Dkt. Juma Malewa(hayupo pichani) alipotembelea Gerezani hapo
Muonekano wa nje wa Gereza la Mahabusu Morogoro ambapo gereza hilo
linauwezo wa kuhifadhi Wafungwa na Mahabusu 144. Picha zote na mdau Lucas Mboje wa
Jeshi la Magereza.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...