Muuguzi katika kituo hicho cha St. Laurent Diabetes Centre, akimpima Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dk. Alex Malasusa huku Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Hussein Mwinyi akishuhudia.
 Wananchi mbalimbali wakipata huduma ya kupimwa ugonjwa wa sukari katika kituo hicho cha St. Laurent Diabetes Centre
Burudani kutoka Mjomba Band ikitolewa
******
Ugonjwa wa Kisukari umekuwa tishio kwa mataifa mengi duniani, Tanzania ikiwemo. Inasemekana kuwa nchi maskini na zinazoendelea duniani ndio zinazongoza kwa ugonjwa wa Kisukari. Aidha, kwa sasa ugonjwa wa Kisukari unashika nafasi ya tatu duniani kueneza vifo.

Katika makala hii, Mtaalam  wa Maradhi  ya Kisukari , Dkt. Mary Mayige , kutoka kituo cha Kisukari cha St. Laurent Diabetes Centre, jijini Dar es Salaam anaeleza kwa ufasaha dalili za ugonjwa huu, kinga na tiba yake.

Dkt. Mary Mayige  anafafanua kuwa Kisukari kwa kifupi (na kwa lugha ya kueleweka) ni ugonjwa unaotokana na kuwa na kiasi kikubwa cha sukari kwenye damu. 

Aliongezea kuwa sukari inapokuwa nyingi kwenye damu ya binadamu, hapo ndipo mtu huyo husumbuliwa na maradhi hayo.

Mkurugenzi  Mtendaji wa kituo cha Kisukari yaani St. Laurent Diabetes Centre, Dkt. Mary Mayige aliwakaribisha watanzania wote katika upimaji wa bure wa Kisukari na pressure katika kituo chao kilichopo Msasani karibu na CCBRT, Dar es Salaam tarehe 10/11/2013. Kabla ya uzinduzi rasmi wa kituo hicho, watanzania walijitokeza kwa wingi kupima na kujua afya zao siku hiyo na kujipatia ushauri wa bure kutoka kwa madaktari na wauguzi wa kituo hicho.

Watu wengi walinufaika na huduma zilizotolewa na kitu hicho cha St.Laurent Diabetes Centre.

Siku moja kabla ya maadhimisho ya siku ya Kisukari Duniani, kituo cha St. Laurent Diabetes Centre walifanya uzinduzi rasmi wa kituo chao Wakiongozwa na mgeni rasmi Mkuu wa Kanisa la KKKT Askofu Dkt. Alex G. Malasusa, pamoja na Waziri  wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dkt .Hussein Mwinyi, na  Naibu Waziri wa Sayansi na Teknolojia Mhe. January Makamba na waheshimiwa wageni waalikwa wawakilishi kutoka serikalini, kwenye  sekta binafsi , za umma na sekta za afya.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. Ni vizuri sana. But it's about time all these facilities base on other regions than Dar. Jamani Tanzania ni nchi kubwa, gharama ni kubwa sana kwa wahitaji wa mikoani, kila wakihitaji huduma nzuri basi ni lazima wasafiri hadi Dar. Everybody can not live i Dar. Hivyo basi Resources ni lazima ziwe distributed for easy axcess. Watu wa mikoani tunawasahau kama kila better facility itapatikana Dar tu.

    ReplyDelete
  2. It is sad that there is a dramatic increase of type 2 diabetes in developing countries, Tanzania being one of them. Sedentary life style and overeating being the major contributing factors to Obesity and consequently type 2 diabetes. There are still a lot of tropical diseases hampering sustainable economic development in Africa (in form of early deaths, days off work etc.). Let us try not to get fat, middle Class Africans can you hear me? anyone with a BM > 30 needs to be screened for diabetes, and in some cases those with impaired glucose tolerance, or at times those with confirmed diabetes, can reverse it if they follow strict dietary and exercise regime, alternatively there a host of medication to use, but the bottom line is we all should avoid getting fat at all cost, if we are already fat, let us do something about the excessive weight.
    Dr Bitozi.

    ReplyDelete
  3. Dr. Bitozi,
    Being fat is part of our culture and it is promoted. We will need a huge education programs to change this mentality. It is not had to see all honorable ministers, member of parliaments and all other leaders with huge abdominal obesity. If you are healthy people will associate you with health problems...go figure.

    ReplyDelete
  4. Mdau wa tatu,I totally agree with you, being fat is considered okay in or culture and is associated with good health and prosperity, HIV-AIDS did not do us a favour at all, as no one wanted to be thin and word will soon spread that "ameukwaa", but we are better than this and we need mass educate the population about the ill effects of obesity.
    Dr Bitozi.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...