![]() |
Naibu Katibu Mkuu wa Shirikisho la
Michezo Wizarani
Bw.Moshi Makuka
|
Naibu
Katibu Mkuu wa Shirikisho la Michezo la Wizarani (SHIMIWI) Bw. Moshi Makuka
amesema shirikisho hilo linatarajia kufanya mkutano wa tathmini wa mashindano
ya SHIMIWI ya mwaka huu mjini Morogoro tarehe 13 na 14 Desemba, 2013.
Akiongea
ofisini kwake Bw.Makuka alisema kuwa lengo kuu la mkutano huo ni kujadili
changamoto zilzojitokeza kwenye mashindano ya mwaka huu.
“Lengo
ni kujadili changamoto zilizojitokeza katika mashindano ya SHIMIWI ya mwaka huu
na kuzipatia ufumbuzi kwa ajili ya kuboresha michezo ya mwaka ujao” alisema
Bw.Makuka.
Aidha,Bw
Makuka aliwataka Wenyeviti wa vilabu,Makatibu wa Vilabu na Maafisa Michezo
kufika bila kukosa ili kukuza michezo serikalini.
“Wenyeviti,Makatibu
na Maafisa Michezo wa vilabu wahudhurie kwa wingi ili waje kutoa changamoto zao
walizokutana nazo katika michezo ya mwaka huu” alifafanua Bw.Makuka.
Shirikisho
la Michezo Wizarani (SHIMIWI) kila mwaka huandaa michezo inayowakutanisha
watumishi wa serikali kutoka katika Wizara,Idara zinazojitegemea,Wakala wa
serikali na Ofisi za Wakuu wa Mikoa ambapo kwa mwaka huu yalifanyika mjini
Dodoma kuanzia tarehe Septemba 21 hadi Oktoba 5.
Wajumbe wanaotakiwa kuhudhuria mkutano huo ni Mwenyekiti, Katibu na maafisa michezo wote kutoka vilabu vya SHIMIWI. Hadi sasa mikoa ya Dodoma na Kilimanjaro imeshatuma maombi ya kushiriki, na mikoa mingine inahimizwa kufanya hivyo mapema iwezekanavyo>
Wajumbe wanaotakiwa kuhudhuria mkutano huo ni Mwenyekiti, Katibu na maafisa michezo wote kutoka vilabu vya SHIMIWI. Hadi sasa mikoa ya Dodoma na Kilimanjaro imeshatuma maombi ya kushiriki, na mikoa mingine inahimizwa kufanya hivyo mapema iwezekanavyo>
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...