Na Abdulaziz Video, Lindi
Wananchi wa wa vijiji vya Singino wilayani Kilwa mkoani Lindi
wamelalamikia Baraza la Taifa la Usimamizi wa Mazingira(NEMC )kwa
kitendo cha kutokusimamia vyema kazi iliyopewa na Bodi ya Korosho
Tanzania katika zoezi la uteketezaji kemikali zilizotelekezwa kwa
zaidi ya miaka 20 zinazosadikika kuwa sumu inayoweza kuathiri afya ya
binadamu, mifugo na mimea.
Akizungumza kwa niaba ya wananchi hao Diwani wa kata ya Kivinje, Bw. Jafari
Arobaini na Mwenyekiti wa kijiji cha Singino Maulidi Mbulula walisema
kitendo cha mkandarasi kumwaga ovyo dawa hizo kunaweza kusababisha
madhara makubwa kwa wananchi,mifugo na mimea na kuathiri kukua kwa mji
huo.
Pamoja na zoezi hilo kusimamiwa na watu wa mazingira lakini bado
zoezi linaonyesha kutotekelezwa kama lilivyopangwa katika makubaliano
ya pamoja kati ya serikali ya kijiji, halmashauri, na NEMC baada ya
kukutwa kemikali hizo zikiwa zimemwagika njiani
Bw. Bakari Mussa Mkazi wa kilwa Masoko ambae alipata kazi katika ghala
hilo alieleza athari alizoziona na kuacha kazi hiyo kulinda afya yake
huku Abdu Saidi mjumbe wa Singino ameomba uongozi wa wilaya
kusimamisha zoezi ili kunusuru maisha ya wananchi wa eneo hilo
kutokana na ukiukwaji unaoonekana sasa kazi inavyoendelea.
Kwa upande wake Afisa msimamizi mazingira NEMC Jorome Kayombo alisema
kuwa awali NEMC ilimwagiza mkandarasi kuchimba shimo futi tano na
kutandika kapeti chini, pembeni na juu ili kuzuia mwingiliano wa
kemikali hizo na udongo huku akikataa kupigwa picha na kutoa ufafunuzi
zaidi wa kemikali hizo kwa madai si msemaji wa NEMC
Katika hali isiyo ya kawaida Uongozi wa ghala hilo ulimwamuru mlinzi
kutoruhusu waandishi kuingia kuangalia hali ya utoaji wa madawa hayo
ghalani kufuatia malalamiko ya vibarua wanaofanya kazi hiyo hatarishi
Eneo la uteketezaji kemikali hizo
Mkaazi wa maeneo ya Singino wilayani Kilwa mkoani Lindi akionesha hali ilivyo
Mmoja wa mifuko ukiwa umeanguka chini
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...