Marehemu Jerry Mruma alikuwa mwanafunzi wa uzamili katika chuo kikuu cha kimataifa cha USIU Nairobi alikutwa alhamisi iliyopita katika chumba cha maiti mjini Nairobi baada ya kuripotiwa kupotea tangu Jumamosi iliyopita.
Jerry alikuwa mmiliki wa kampuni ya Kilimo yetu akiuza hisa za Kilimo kijana huyu mtanashati na mwenye akili ya biashara alikuwa akisoma wakati huo huo akifanya biashara hii iliyopata umaarufu sana huko nchini Kenya.
Kwa mujibu wa ripoti ya Polisi na kamera za CCTV ni kwamba Jerry alionekana hai mara ya mwisho saa tano na dakika tisa usiku alipokuwa akitoka kwenye hafla ya usiku wa Mtanzania aliyokuwa ameandaa katika hoteli ya Sarova.
Aliondoka hotelini hapo kwa miguu akiwa peke yake na kwa mujibu wa Chuo hicho alituma ujumbe wa mwisho kwa rafiki yake wa kike mnamo saa 5 na dakika 38 za usiku akimwambia ametoka kwenye hafla hiyo na anaelekea nyumbani kwake.
Jerry aliwahi kufanya mazungumzo na Sauti ya Amerika juu ya kampuni yake Kilimo yetu nchini humo.
Jerry amezikwa Jumanne katika makaburi ya Kinondoni mjini Daressalaam. Chuo cha USIU kimeamua kuanzisha mfuko wa kusomesha wanafunzi kwa jina lake.
Uchunguzi wa awali unaeleza kuwa kijana huyu alipata majeraha ya kichwa na mpaka sasa Polisi wa Kenya wanasema bado wanafanya uchunguzi.
Wanafunzi na wakazi wengi wa jiji la Daressalaam na Nairobi walijitokeza kumzika mwenzao, msiba ambao umeacha majonzi makubwa na simanzi katika familia na kuangalia mazungumzo yake huko Nairobi na GBSTV bofya hapa.
dah!!mungu amlaze mahali pema peponi,what a talent, huu ni moja ya ushaidi kuwa tunaweza soko la east Africa.ni kujiamini
ReplyDeleteThis guy was killed cause his intelligence threatened some people. This guy would be our president, if he was left to live. RIP brother!!!
ReplyDeleteVery Smart., May you RIP East Africa we have lost an excellent talent.
ReplyDeleteKenya ndio walivyo.Inawezekana wamemuua kwa wivu.He could be much further and safe kama angekuwa home.
ReplyDeleteThis is a HUGE loss for Mrumas, Tanzania and the continent. He had great potential and it's a shame his life was stolen from us. May he rest in peace.
ReplyDelete
ReplyDeletewazazi kwanza poleni sana, TANZANIA IMEPOTEZA TUMAINI KUBWA NA ASSET KUBWA KWA KIJANA HUYU, THIS YOUNG MAN COULD HAVE BEEN OUR NEXT OBAMA IN TANZANIA VERY SMART AND WEEL ARTICULATED.
POLENI SANA WAZAZI
MUNGU AWATIE NGUVU.