ZANZIBAR NOVEMBA 15, 2013. Jeshi la Polisi Zanzibar limewakamata watuhumiwa wemgine watatu wakiwemo Maafisa wawili wa Mamlaka ya Mapato nchini TRA kituo cha Bandari Zanzibar kwa kuhusika na kashfa ya kupatikana kwa meno ya tembo yenye thamani ya Mabilioni ya shilingi.
Kamishna wa Polisi Zanzibar CP Mussa Ali Mussa, amewataja Maafisa hao wa TRA waliokamatwa kuwa ni Omari Hamad Ali(50) na Mohammed Hija(48) ambao wote wanafanyia kazi katika Bandari ya Zanzibar. Mtuhumiwa mwingine ni kibarua wa Mamlaka ya bandari Zanzibar Haidar Ahmad Abdallah(54).
Kukamatwa kwa watuhumiwa hao kunaifanya idadi ya watuhumiwa waliokamatwa hadi sasa kwa kuhusika na sakata hilo kufikia watano.
Tayari watuhumiwa hao wamesafirishwa kwenda Makao Makuu ya Polisi Dar es Salaam kwa ajili ya mahojiano zaidi.Pamoja na mambo mengine, kusafirishwa kwa watuhumiwa hao kwenda Jijini Dar es Salaam, kunatokana na Zanzibar kutokuwa na Sheria maalumu inayohusu wanyamapori.
Maafisa wa Idara ya Wanyamapori nchini, leo wamekamilisha kazi ya kuhesabu na kulinganisha vipande 1,023 vya meno ya tembo vilivyokamatwa jana kwenye Bandari ya Zanzibar na kubaini idadi ya tembo waliouawa kuwa ni 305.
Hadi sasa bado Makachero wa Polisi wa Kimataifa Interpol hapa nchini kwa kushirikiana na Makachero wa Polisi Zanzibar, idara ya wanyamapori makao makuu wanaendelea na upelelezi wa kuwabaini wale wote waliohusika na kashfa hiyo.
Jana Kamishna wa Polisi Zanzibar CP Mussa Ali Mussa, alisema kuwa kazi kubwa iliyobaki ni kuhakikisha kuwa upelelezi wa kina unafanyika ili kuwakamata wale wote wanaohusika na mtandao huo.
Alisema hadi sasa Jeshi la Polisi bado linamsaka tajiri aliyewezesha mipango ya kukusanywa na kusafirisha shehena hiyo kutoka Tanzania Bara hadi Zanzibar ili kusafirishwa nje ya nchi.
Si mchezo wanatumalizia tembo wetu
ReplyDeleteWala msihangaike kumtafuta !
ReplyDeleteHuyo tajiri yupo kwao China mustarehe na la ajabu ni kuwa huko kwao na Serikali yao huyachukulia masuala yanayo husu Meno ya Tembo kama Ibada na sio Kosa la Jinai kama huku kwetu Tanzania!
Wachina wengi ni Waumini wa Dini ya Mabuda (Buddhist) hivyo Miungu ya Dini ni mingi sana wana Miungu zaid ya mmoja na pia Miungu hiyo hutengenezwa kwa Pembe za Tembo na Faru.
Tembo 305 ndio walio uwawa kupata mzigo huo ulio kamatwa!!!
ReplyDeleteSasa hapo si ndio ina maana Tembo wa Tanzania wamesha kwisha wote?
Kwa hilo naomba serikali yetu itafakari uhusiano wetu na wachina kwa upya.kuwepo na udhibiti wa visa zao kuingia nchini hawa siyo watu hawa mnaowakumbatia.kuna mambo mengi sana yanaharibika kutokana na ujio wa wachina.
ReplyDeleteSerikali izuie hata hizo sea products kusafirishwa nje kwani kwa mtazamo wangu naona bado ni nyara za Taifa sasa mkizimaliza watoto wetu wataziona wapi na vijukuu?Jamani serikali acheni utani na mali za nchi ambazo baba wa taifa amezilinda miaka yote na angekuwepo asingeruhusu huo upuuzi wa wachina.
ReplyDeleteJamani, contena lina nyaraka zote toka aliyepakia mpaka atakaye pokea.
ReplyDeleteSasa shida ipo wapi??
Acheni michezo ya kuigiza tumechoka na hii tabia ya kusema eti aliyeagiza hajulikani.
Tutuchunguze jina la Consignee na shipper ili tuone kama hawajawahi kutuma mizigo mingine siku za nyuma.
Hao watu ni wazoefu wa miaka,you guys know better!!!!!
Hapo mpaka mabwana pori wanaweza kuwa wamehusika,tunasubiri utafiti wenu...
Nashauri ili kuwanusuru Tembo na Faru wetu waliobaki wachache sana na wanao hesabika kwa idadi yao TUWAHAMISHIE IKULU KWA MHE. RAISI KIKWETE!!!
ReplyDeleteHATUNA JINSI, KWA KUWA MAHARAMIA WAMEWAMALIZA NA SISI TEGEMEO LETU NI KWA BABA YETU MPENDWA RAISI KIKWETE NDIYE MTETEZI WA MWISHO ALIYEBAKI !
Hahahahaha !
ReplyDeleteMdau wa 7 hapo juu umenivunja mbavu!, kwa kweli Tembo na Faru wamefikia hali ya kutisha sana kwa idadi hiyo kuuwawa.
Nadhani hilo kuwahamkishia wanyama Ikulu kwa Mhe. Raisi ni wazo zuri sana, ingawa kwenye Makazi ya Mhe. Raisi nafasi itakuwa ni ndogo kwa viumbe hao kupata nafasi ya makazi mjengoni, isipokuwa kama itakuwa hivyo WANYAMA hawa watapata raha sana na ulinzi wa uhakika na usalama wao kwa kuwa Mhe. Raisi ni mkarimu sana ,sana, sana!
Hilo la kuwahamishia wanyama Ikulu kwa Mhe. Raisi tulifikirie ingawa linakuwa la kufikirika zaidi maana kwa hali ilivyo sasa inatisha sana!
ReplyDeleteTusije kushangaa tukiambiwa ya kuwa Tanzania imemaliza Tembo na Faru wake wote na sasa haina hata mmoja!
Duuu,
ReplyDeleteMdau wa Tisa 9 ni kweli maana Majangili wanawaua Tembo na Faru bila hata kuacha mbegu!
Kuwahamishia Wanyama Ikulu:
ReplyDeleteInawezekana KIDIJITALI Wanyama wakawa wapo Ikulu ilhali wakiwa huko Mbugani.
Nimeona Mwana Malkia Prince Charles na mwanaye William wamevutiwa na wanyama Pori, Mhe. Raisi Kikwete jaribu kuzingumza nao kuhusu wazo hili hapa chini:
..................................
Kinachowezekana ni KUDIJITALIZE Makazi yanaowazunguka na wao Tembo na Faru pia kuwa Digitalized kwa kufungwa CHIP maalum ammapo makazi yao yatakuwa Electronized ambapo kila mnyama atakuwa na Kikadi chake amewekewa endapo anaingia Mkazi asiye thibitika alarm zinalia na anakuwa tracked na kukamatwa.
Iwekwe Mvamizi ameweze kusomeka ktk system akiwa umbali wa 1KM ambay hakuna bunduki inaweza kufika hao.
Hivyo Mhe. Raisi Kikwete kama Mlezi atawekewa Computer maalum itakayo onyesha kila kinacho jiri huko Mbugani kwa Tembo na Faru na HAPO WANYAMA WATAKUWA WAMEHAMISHIWA IKULU KIDIJITALI !!!