Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na Wadau mbali mbali walioshiriki kwenye Warsha ya Kamata Fursa Twenzetu,iliyofanyika leo kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee,jijini Dar es Salaam. Mh. Rais ameupongeza uongozi wa Kampuni ya Clouds Media Group kwa ubunifu wao wa Kampeni ya Fusra inayowakutanisha na kuwahamasisha vijana mbali mbali nchini kujituma na kufanya kazi ili kutokomeza swala zima la ukosefu wa ajira,Pia Rais Kikwete ameahidi kuwasaidia waendeshaji wa Warsha hiyo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Clouds Media Group,Joseph Kusaga akizungumza machache kabla ya kumkaribisha Mgeni Rasmi,Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete,ili aweze kuzungumza na Wadau mbali mbali walioshiriki kwenye Warsha ya Kamata Fursa Twenzetu,iliyofanyika kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee,Jijini Dar es Salaam.
Njia hizo za kuhamasisha jamii ndizo zinaleta maendeleo ya kweli nilikukwa nalilia Raisi wangu kuwa na nafasi ya kuhamasisha jamii direct sasa naamini mabadiriko yataonekana Tanzania Heko Luge
ReplyDelete