Tarehe 24 Nov 2013 Swahili Fashion Week walifanya mchujo wa kutafuta wanamitindo mbalimbali ambao wataonesha mavazi ya wabunifu katika wiki ya maonesho ya mavaz ya swahili kuanzia tarehe 5 dec hadi tarehe 8 dec 2013, wanamitindo mbalimbali walijitokeza kwa wingi kutaka kushiriki kwa namna moja na nyingine katika maonesho hayo.
Mgeni rasmi alikuwa Herrieth Paul ambaye ni mwanamitindi maarufu Mtanzania mwenye makazi yake nchini Canada, waliohudhuria maonesho hayo pia alikuwapo Jamillah Vera Swai,(Mbunifu wa Mavazi), Gabriel Mollel (Mbunifu wa mavazi), Pedaiah John (Mbunifu wa Mavazi), Honest Arroyal (Mratibu wa mitindo na ubunifu SFW), Mustafa Hassanali (Mwanzilishi wa Swahili Fashion Week) na Esi Mgimba (Afisa Habari na Mahusiano SFW)
Wanamitindo wa kike katika mchuzjo wa pili
wanamitindo wa kike wakijiandaa kuonesha uwezo wao wa kutembea
jukwaani katika mchujo wa pili
wanamitindo wa kiume wakionesha mbwembwe zao za kutembea
jukwaani katika mchujo wa pili.
wanamitindo wa kiume wakiwa katika mchujo wa tatu
wanamitindo wakimsikiliza mwanamitindo maarufu duniani ...
H. Paul ambaye alikuwa mgeni rasmi katika mchujo huo
jopo la majaji wakijadiliana jambo kuhusiana na wanamitindo
waliopita katika mchujo
GOOD LORD THOSE GUYS ARE HOOOOOOOOOOOT. IS THAT TANZANIA? WOW AM IMPRESSED WITH HOT TZ GUYS MAN!
ReplyDelete