Wageni mbali mbali wakiwa wamefurika kwa wingi kwenye Banda la Wanafunzi wa Kitanzania wanaosoma katika Chuo Kikuu cha East China Normal University (ECNU) kilichopo mjini Shanghai wakati wa Maonyesho ya wanafunzi mbalimbali wa kigeni Katika Chuo hicho,ambapo hupewa mabanda ili waoneshe vitu asilia na mambo mbalimbali yahusuyo nchi yao kwa ujumla.
Mmoja wanafunzi wa Kitanzania katika Chuo Kikuu cha East China Normal University (ECNU) kilichopo mjini Shanghai akimuonyesha mgeni alietembelea banda hilo picha mbali mbali.
Baadhi ya Wanafunzi wa Kitanzania wanaosoma katika Chuo Kikuu cha East China Normal University (ECNU) kilichopo mjini Shanghai wakiwa kwenye picha ya pamoja.
Huo ndio uzalendo unaotakiwa kufanywa na kila mtanzania aliepo ugaibuni mtu kwao bwana asikwambie mtu,,hiyo kofia tu bao la kisigino kwa wengine,pongezi sn kwenu ndugu zangu
ReplyDeleteKweli Vijana wa Tanzania huko China mmeibeba vyema nchi yetu!
ReplyDeleteHongera sana kwa Uzalendo!!!!
Tuwe na Utamaduni wa kufuatilia jinsi watu wanavyo jituma kwa ajili ya kuibeba Bendera ya nchi!
ReplyDeleteTuwe na utamaduni wa kuwapenda wenye moyo wa Uzalendo na kujituma na sio moyo wa ubinafsi na Biashara.
Hivi jamani kwa nini tusipeane Uongozi kwa vigezo?, mfano Vijana hawa wakirejea nchini baaday ya Masomo yako nje kwa nini wasipewe Kipaumbele kwenye nafasi za Uongozi?
Ni vile wanaonekana wana nia njema na nchi hivyo wakishika nyadhifa ni wazi pia wataitendea vyema nchi !
Daah!nimeipenda hii... Kwa kweli kama Serikali inasoma na kupitia hii blog basi nimatumaini yangu wameshaona nini cha kufanya kuzidi kuwatia moyo vijana hawa... Hongereni sana ndugu zetu huko...
ReplyDeleteWametisha
DeleteBig up bro and ur fellows
ReplyDeleteAm so proud of you.
Sina hakika sana kama vitu kama hivi vinapewa shavu na wizara husika ili kuhakikisha nchi yetu inatangazwa na kuimarisha uhusiano wa kimataifa lakini zaidi sana kuwa nafasi ya kuvutia watalii kuja kutembelea vuvutio vya kitalii hapa Tanzania.
Hongereni sana wakuu
Mnaonekana mna hari na mnafurahia mnachokifanya.
ReplyDeleteMmenibamba vilivyo.
Hivi ndivyo vitu tunavyovitaka kusikia na kuona vikifaanywa na vijana wetu wa Kitanzania wakiwa nje ya nchi.
Hongereni kwa uzalendo wenu.
Natumaini serikali yetu inaliona hili.
Yaani mmenikosha hadi raha.
Asante Michuzii kwa kutupa hamasa hii katika picha.
Kizalendo zaidi.
ReplyDeleteHongereni vijana.
Kazi nzuri
Vijana wametisha sio siri, wanastahili pongezi!
ReplyDeleteAiseeee! Hawa vijana ni mashujaaaaaa.. mh. Rais inabid aipate hii. Mmetutendea vyema ndugu zetu na milele mtakua mashujaa kwa kupeperusha bendera ya nchi yetu nzur. Mnastahil kupongezwa pind mrudipo nchini. Majina ya hwa vijana yatajwe na yapelekwe mbele serikal iwatambue hawa watu. Daaah sijui hata niseme nn. Mbarikiwe sanaaaa......
ReplyDeleteMichuzi asante sana kea kutupa hii raha ya wtz wenzetu wanaofanya vyema huko mbele.
ReplyDeleteVijana wanaopenda nchi yao. Big up brother MWM na timu nzima hapo shanghai. U truely Tanzanian and we are proud of you.
ReplyDeleteYou made my day guys and all the best katika masomo yenu......
These guys are patriots. Wako wapi vijana wengine wanamna hii. Wangeiweka Tz kwenye raman mpya. Thank yu broz. Thanx michiz kwa kaz nzur.
ReplyDeleteUnajua inashangaza kuona wapo wazalendo na wapenda nchi yetu kiasi hik. Sijui serikali itasema nn juu hawa vijana. Kiukweli wanastahili pongez. Wako ugenn lakin hawasahau asili, nimeona hapo mpaka sukar n majan ya chai ya tz. Asante sana ndugu zetu hata km serikali haitaona hii watz tumeona..... michuzi asante kwa kututendea haki na kuweka hiz picha ww ni wa ukwelii aisee...
ReplyDeletenimefurahi sana kuona vijana,,tena wasomi kuitangaza nchi yao kwa kweli nimefurahi sana kwa mimi binafsi
ReplyDeleteHongereni sana. Uzalendo ni kitu cha kujivunia. Mmeipeperusha bendera ya Tanzania vizuri.
ReplyDeleteSaafiii saanaaa. Tanzania ni nchi yetu na Afrika ni moja.
ReplyDelete