Miongoni mwa vitendo vinavyoshamiri Makete vya watoto kujihusisha na biashara ya kuuza mkaa
Mkaa ukisubiri wateja.
-------
Na Edwin Moshi,Makete.
Mafunzo
ya ulinzi na usalama wa mtoto dhidi ya ukatili na unyanyasaji
yaliyoanza jana wilayani Makete mkoani Njombe yanaendelea katika ukumbi
wa Sumasesu Tandala
Mafunzo
hayo yaliyofunguliwa na Afisa Ustawi wa Jamii wilaya ya Makete Bw.
Leonce Panga yameshirikisha wadau mbalimbali wakiwemo viongozi wa dini,
dawati la jinsia kutoka kituo cha polisi Makete, maafisa elimu,
mwanasheria, magereza, wauguzi, madaktari pamoja na hakimu mfawidhi wa
wilaya ya Makete
Katika
mafunzo hayo yanayowezeshwa na Bi Asha Mbaruku pamoja na Ramadhani
Yahaya kutoka ustawi wa jamii makao makuu jijini Dar es Salaam wamesema
kuwa lengo la mafunzo hayo ni kuwajengea uwezo wadau hao namna ya
kuwahudumia watoto wanaokuwa wamefika kwenye ofisi zao kupata msaada
endapo anakuwa amepata tatizo akitolea mfano kufukuzwa shule kwa kukosa
ada
Wamesema
washiriki hao wanapaswa kuwa timu ya ulinzi na usalama wa mtoto ili
waweze kumsaidia mtoto, huku Bi Asha akisisitiza kuwa kuna huduma ya
msaada kwa watoto wanaofanyiwa vitendo vya ukatili iliyoanzishwa
wizarani inayoitwa huduma mtandao (Child helpline) inayohusu mtoto
kupiga simu moja kwa moja na kueleza shida yake na kupatiwa suluhu
Washiriki
pia wamefundishwa njia mbalimbali za ufundishaji wa masuala ya ulinzi
na usalama wa mtoto kwa ngazi ya chini ya serikali
Kwa
upande wao washiriki wametoa visa mbalimbali vinavyoendelea katika
jamii ya Makete ikiwemo kata ya Mbalatse ambayo watoto wa kike
wanafanyiwa vitendo vya ukeketaji kwa siri kubwa
Mafunzo
hayo yameweka wazi hatua zinazochukuliwa na serikali kupambana na
vitendo vya ukatili kwa watoto ikiwemo kutunga na kusimamia sheria
mbalimbali zinazomlinda mtoto
Mafunzo
hayo ya siku 5 yaliyoanza jana yameandaliwa na ustawi wa jamii makao
makuu jijini Dar es Salaam na yanatarajiwa kuhitimishwa Jumamosi wiki
hii
Wanyalu Wilayani Makete.
ReplyDeleteOhhhh Sarafu mnaichungulia vibaya sana, watoto badala ya kuwapeleka Shule kusoma mnawakabidhi Mikaa kuuza?
Sasa wakale wapi? Wazazi wao wahahitaji msaada, wao wako shambani, watoto wanauza mkaa nyumbani. Msitake kuiga mambo ya ughaibuni. Wao wanawapa watoto "child benefit" na wazazi "unemployment benefit" kwa hivyo hakuna sababu ya watoto kunyanyaswa.
ReplyDeleteNi matokeo ya ubinafsi wa viongozi.
ReplyDeleteKwani Tanzania inashindwa kuwa benefit kama za ulaya wakati nchi ina kila utajiri kutoka kwa mwenyezi mungu?
Ni uroho wa utajiri kwa walio juu kushindwa kutatua haya matatizo ambayo si kweli kwamba nchi yetu haina uwezo kuyatatua.
Tutabakia hivihivi mpaka mungu atuangamize au atutie majaribu makubwa, labda ndio tutakumbuka.
System ya nchi ipo corrupted,period!
ReplyDeleteUlaya na TZ kwa sasa ni sawa tu.Tuna wasomi,migodi ya madini, gas, wanyama, bandari,tunalipa kodi nk nk.
Tuna taka nini tena tuweze kujikwamua ? Tatizo ni kuwa kila mradi kuna 10% ya watu wajanja.
Walio juu wamejisahau kuwa kuna watu hata mlo mmoja hawana.
Pato la Taifa ni kwao wao na familia zao na si haki ya kila mwananchi.
Ulaya na Marekani shule ni bure (primary to high school including breakfast na lunch)na mtoto kama hajaenda shule mzazi unashitakiwa na kupelekwa mahakani.