WAZIRI MKUU Mizengo Pinda amewataka maafisa mipango miji nchini kurekebisha utendaji wao wa kazi ili waweze kubadili taswira mbaya iliyojengeka miongoni mwa jamii dhidi yao.

Ametoa kauli hiyo huo leo mchana (Alhamisi, Novemba 27, 2013) wakati akifungua Mkutano wa Kwanza wa Wataalam wa Mipangomiji waliosajiliwa na Bodi ya Usajili wa Wataalam wa Mipangomiji ulioanza leo jijini Dar es Salaam.

“Taswira ya utendaji kazi katika taaluma ya mipangomiji na katika  sekta  ya  ardhi  kwa  ujumla miongoni mwa wananchi na Serikali siyo nzuri sana. Watafiti wanatueleza kuwa kati ya asilimia 60 na 80 ya makazi kwenye miji  yetu hapa nchini yamejengwa kiholela. Na kwa kiwango hicho hicho wakazi wa mijini wako kwenye makazi hayo na wanaishi kiholela,” alisema.

“Wako wanaosema ninyi ndiyo chanzo cha hiyo migogoro, wako wanaosema ninyi kwa rushwa ndiyo wenyewe, mimi sishangai madai haya ila ninawasihi muwe na roho ngumu katika kushinda vishawishi hivi,” alisisitiza.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Can not overemphasize the Prime Miisters observations. Have been in Geita for almost a month on official asignment yaani najiuliza maswali ni jinsi gani huu mji wa mkoa mpya wa Geita utakavyojipanga ili kupata tafsiri halisi ya Mkoa. Hapa katikati kwenye barabara kuu pekee na vitongoji pembezoni ni tafrani tupu. Makazi holela, uchafu na msongamano.
    True by large lawama ni mipango miji lakini we can not run from the truth that kwa asili watanzania ni wachafu na hawana ustaarabu.

    ReplyDelete
  2. The mdudu K, anauliza hivi ni nn maana ya MATOKEO MAKUBWA SASA? Kwajinsi nilivyo muelewa RAIS wetu kuhusiana na hili neno ana maana ya kwamba 1,vijiji vyote ndani ya Tanzania kama vilikua havina UMEME,MAJI,MAHOSPITAL MAPYA,MASHULE MAPYA,MABARABARA YA KISASA,NYUMBA ZA KISASA na zijengwe kimpangilio unaotakiwa,MATOWN YA KISASA na yasiokua na mifoleni ya kufa mtu,NJIA ZA RELI ZIWE KUBWA NA ZA KISASA,MABANDARI YA KISASA NA YAWE MAKUBWA,MA UDOM YAWE YA KUMWAGA,WALIMU WALIPWE VIZURI,MADAKITARI PIA,WAFANYA KAZI PIA,HATUTAKI RUSHWA,,,jamani ndugu zangu watanzania hiyo ndio mipango ya RAIS wetu na ndio tafsiri ya neno MATOKEO MAKUBWA SASA na sivinginevyo,,sasa why bado watu wanafundishana cha kufanya? Jamani mtu yeyote yule asie fahamu maana ya MATOKEO MAKUBWA SASA tunamuomba akae pembeni,coz tunataka Tanzania ya kwenda mbele tu,nawaombeni sn wadau wote wa ndugu MICHUZI mnikosoe nilipo kosea na tuwe pamoja nilipo wagusa,,nina mengi sn ya kuchangia ili Tanzania yetu iende tunapopataka,,ila kwa leo naishia hapa.amani kwenu watanzania wote popote mlipo

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...