Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Visiwani Comoro, Mhe. Chabaka Kilumanga, leo tarehe 3 Desemba 2013 amewasilisha Hati za Utambulisho kwa Mhe. Dkt. Ikililou Dhoinine Rais wa Muungano wa Visiwa vya Muungano wa Comoro. 
Katika hafla hiyo iliyofanyika katika Ikulu ya Beit Salaam, Mhe. Balozi Kilumanga na Mhe. Rais Dhoinine walipata fursa ya kuzungumza machache katika muktadha wa kuimarisha uhusiano wa kihistoria na kindugu uliopo kati ya Tanzania na Comoro kwa manufaa ya wananchi wa nchi hizo. Hafla hiyo ilihudhuriwa pia na viongozi mbalimbali wa Serikali ya Comoro pamoja na maafisa wa Ubalozi wa Tanzania mjini Moroni.
Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Visiwani Comoro, Mhe. Chabaka Kilumanga, akiwasilisha Hati za Utambulisho kwa Mhe. Dkt. Ikililou Dhoinine Rais wa Muungano wa Visiwa vya Muungano wa Comoro mjini Moroni leo. 
Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Visiwani Comoro, Mhe. Chabaka Kilumanga, leo akiongea na  Mhe. Dkt. Ikililou Dhoinine Rais wa Muungano wa Visiwa vya Muungano wa Comoro baada ya kuwasilisha hati za utambulisho katika Ikulu ya Moroni, leo. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...