Katibu wa NEC,Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiro akipongezwa na Katibu wa NEC-Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye kwa kuteuliwa na Rais Jakaya Kikwete kuwa Mbunge, jioni mjini Mbalizi, jijini Mbeya. Viongozi hao wamo kwenye ziara ya kuimarisha chama na kukagua miradi ya maendeleo inayotekelezwa kwa kuata Ilani ya Uchaguzi ya CCM. Akizungumzia uteuzi huo, mjini Mbalizi jioni hii, Dk. Migiro amemshukuru Rais Jakaya Kikwete kwa uteuzi huo ambao ameupokea kwa furaha, na kueleza kuwa kitendo hicho kinadhihirisha jinsi Rais Kikwete alivyo na imani naye pamoja na imani kwa Wanawake wa Tanzania
Dk. Migiro (kulia), akipongezwa na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana kwa uteuzi wake huo.
Dk. Migiro akizungumza na vyombo vya habari, jinsi alivyopokea kwa furaha uteuzi wake huo.
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Abbas Kandoro akimpongeza Dk. Migiro kwa kuteuliwa na Rais Kikwete kuwa Mbunge.
Hongera mh Asha kwa kuteuliwa na mh Raisi kuwa mbunge kwa kweli unastahili hasa nilikuwa nakufuatilia unavyochapa kazi kadi inanipa moyo hasa nilivyokuona umepanda ngazi unaonyesha mfano na hiyo ziara ya Kinana si mchezo kwani ni sawa na kuwa jkt.Tanzania inahitaji huo uchapa kazi haihitaji miungu inayokaa maofisini kwani mawaziri wa JK karibia wote ni miungu kwenye suti na viti vya kuzunguka ila umeonyesha mfano kwa kula kila aina ya chakula na maskini huwezi amini kuwa ndo ulikuwa UN.God bless you.
ReplyDeleteSijui kwa nini huwa kila nikimtazama Mama Migiro huwa naona maandishi makubwa " VICE PRESIDENT OF THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA 2015 - 2025 " Mungu amjalie
ReplyDeleteMr Emmanuel hapo juu, maono yako ni sahihi, ila umeona nusu picha, kama ni ndoto basi imaishia kabla ya kuisha ndo ukashtuka uzingizini. Huyu mama, ndo anatembezwa na Ndugu Kinana kwa ajili ya 2015. Huyu ndo JK's choice for CCM presidential candidate 2015. Take my words.
ReplyDeleteMi nawaangalieni tu wadau hapo juu mnaotoa maoni kama hamjui siasa chafu zilizoingia TZ, vita vilivyopo ndani ya CCM ni kubwa kuliko hizo ndoto zenu za alfajiri ambazo unaweza ota upo TOKYO ukishtuka unajikuta Magurumbasi, wao wanapoendelea na kampeni kupitia kauli mbiu KUIMARISHA CHAMA wengine wanaendelea na kampeni kama za HARAMBEE, ZIARA ZA BURUNDI NA KONGO, VITA DHIDI YA MADAWA KATIKA VIWANJA VYA NDEGE, UZINDUZI WA BARABARA...nk, yaani kila mmoja na sekta yake na JK hana sauti kama ilivyokuwa JKN hasa ikikumbukwa yeye mwenyewe almanusura apokwe uenyekiti wa hicho chama anachokiongoza, sa angalieni vizuri KAMBI ZINAVYOCHAKARIKA halafu mtajua ni kambi ipi ya JESHI LA MTU 1 inavyopata nguvu ya hatari hivi sasa...!
ReplyDeleteMkae mkijua Mama Migiro anauzwa ili afahamike period.
ReplyDeleteMdau
Columbus,Ohio