Na Abdulaziz Video,Lindi
Katika kulinda na kutetea ikiwemo kuendeleza maslahi ya mwanachama wa
Mifuko ya hifadhi ya jamii Nchini,Mamlaka ya Usimamizi wa sekta ya
Hifadhi za Jamii(SSRA)Imetoa mafuno kwa viongozi na waajiri Mkoani
Lindi ili kutekeleza sheria iliyounda mamlaka hiyo na kuhakikisha
huduma bora zinamfikia kila Mtanzania
Akifungua mafunzo hayo,Mkuu wa Mkoa wa Lindi Ludovick Mwananzila kuwa
Serikali inaandaa utaratibu maalumu utakaowawezesha wanachama wa mfuko
husika kunufaika nao wakiwa kazini ama baada ya kumaliza utumishi wao.
Pia amewasisitizia wafanyakazi nchini kuwa suala hilo limepewa
kipaumbele ili kupatiwa ufumbuzi haraka iwezekanavyo. Huku akiwasihi
wafanyakazi wenye mawazo ya kuacha kazi ili tu wachukue mafao yao ya
kujitoa kuachana na fikra hizo potofu ambazo alisema zitaleta athari
kwa familia zao.
Pamoja na Rai hiyo Mwananzila aliwataka SSRA kuhamasisha Mifuko ya
Hifadhi za Jamii kutembelea mara kwa mara wanachama wao ikiwemo kutoa
elimu ya mafao/Mikopo ambapo kufanya hivyo kutasaidia watumishi
kujipanga baada ya kustaafu kuliko sasa mtumishi anachukia kustaafu
“Jamani tunashuhudia wengi wanaona kustaafu ni kukaribia kifo na
utumia mbinu nyingi kukwepa hilo kumbe kupitia Mifuko hii sasa ni
mkombozi wa maisha ya wastaafu ila ni wazi kuna mifuko mingine ni
kandamizi kwa mstaafu na haitoi fursa kwa mtumishi kushawishika
kujiunga….”Alimalizia Mwananzila.
Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano wa mamlaka hiyo Sarah Kibonde Msika
akitoa mada katika mafunzo hayo alieleza kuwa SSRA imetoa miongozo
sita (6) kwa lengo la kuhakikisha sekta ya hifadhi ya Jami inakuwa
bora na endelevu itakayo boresha wanachama wa sekta ya hifadhi ya
jamii kama ilivyoainishwa kwenye sheria na kufafanua kuwa miongozo
hiyo pia itasaidia kuhakikisha mwanachama anapata haki yake
anayostahili kwa wakati muafaka na kuondoa migongano baina ya
mifuko,waajiri na waajiriwa.
Pia Miongozo hiyo itahakikisha uwekezaji wa mifuko unaleta maendeleo
bila kuhatarisha afya ya mifuko na utawala bora unaziongatiwa katika
shughuli zote za uwekezaji kwa manufaa ya mifuko,wanachana na Taifa
kwa Ujumla.
‘Mamlaka inategemea kuwa katika kipindi kijacho sekta ya hifadhi ya
jamii itakuwa endelevu,yenye mafao bora na mifuko ya hifadhi ya jamii
itaongezeka. Kwa kuwa mamlaka inao uwezo wa kuchukua hatua za
kinidhamu ikiwa pamoja na kutoa adhabu kwa wasimamizi na wadhamini wa
mifuko kwa kutotekeleza matakwa ya sheria”Alieleza Kibonde alipokuwa
anamalizia mada yake
Mada nyingine katika Mafunzo hayo iliwasilishwa na Mkurugenzi wa
Sheria SSRA,Bw Ngabo Patrick ambapo alieleza mafanikio na changamoto
pamoja Muelekeo wa SSRA Ikiwa pamoja na kuendelea na mpango wa
kuwianisha na kuhuisha mifuko ya hifadhi ya jamii ili kuhimiza
wanajamii wengi zaidi kuingia katika mfumo wa hifadhi za jamii na
kutopoteza haki zao pale inapobidi kuondoka katika mifumo hiyo
Mafunzo ya Siku moja yamefanyika mjini Lindi ambapo pia baadhi ya
Changamoto ilibainika ni vema Elimu Hiyo pia ikifikishwa kwa watumishi
wa kada ya chini kupitia Mifuko ya Hifadhi pamoja na Mamlaka hiyo
Mkuu wa Mkoa wa Lindi akifungua Mafunzo kulia ni Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Lindi Abdul Dachi na kushoto kwake ni Mkurugenzi wa Sheria SSRA,Ngabo Patrich
Baadhi ya Viongozi wakisiliza Mada zilizokuwa Zikiwasilishwa na Mamlaka ya Usimamizi wa Sekta za Hifadhi za jamii katika Ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Lindi
Mkuu wa mawasiliano na uhamasishaji,Bi Sarah Kibonde Msika akiwasilisha mada kuhusiana na malaka ya SSRA
Katibu wa Tughe Mkoa wa Lindi,Bi Frola Urassa akitaka apewe Ufafanuzi kuhusiana na Tofauti ya mafao yanayotolewa na mifuko ya Jamii
Mkuu wa Mkoa wa Lindi Ludovick Mwananzila akiwa katika Picha ya pamoja na watumishi wa Ofisi yake pamoja na watumishi wa SSRA.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...