Na Nathan Mpangala
Help for Underserved Communities Inc. (HUC), imefadhili wanafunzi 11 kutoka mikoa ya Dar es Salaam, Mbeya na Morogoro kozi mbalimbali za ufundi zinazotolewa VETA, ambapo baadhi yao wameshaanza mafunzo na wengine wanatarajiwa kuanza Januari mwakani.
Akizungumzia ufadhili huo, Rais wa asasi hiyo, Bi. Zawadi Sakapalla – Ukondwa, alisema, “ufadhili umelenga vijana wenye nia ya kujiendeleza lakini wamekuwa wakishindwa kufanya hivyo kutokana na uyatima na wazazi au walezi kutokuwa na uwezo wa kuwasomesha”.
Majina, kozi na mikoa wanayotoka vijana hao ni; Joseph Mboya, Saidi Makope, Yasini Musa (ufundi magari, Dar es Salaam), Neema Bungara (umeme wa magari, Dar es salaam), Francis Mustafa (ufundi magari, Morogoro), Hassan Bakari, Fadhili Munda (udereva, Dar es Salaam), David Mwasyeba (udereva wa pikipiki, Mbeya), Jamila Mwenda (usekretari/kompyuta, Dar es Salaam), Monica Mhelela (saluni na utengenezaji nywele, Dar es Salaam) na Rose Mawawa (ufundi cherehani, Dar es Salaam).
HUC ni asasi isiyo ya kiserikali yenye makao yake Marekani, inayosaidia upatikanaji wa maji safi na salama ya kunywa, maktaba za kijamii na vifaa vya elimu kwa maeneo yenye upungufu wa huduma za kujamii. Habari zaidi: https://www.facebook.com/pages/Help-for-Underserved-Communities-HUC-USA/412893725452394
Baadhi ya vijana waliopata ufadhili wa kozi mbalimbali za ufundi toka Help for Underserved Communities Inc. (HUC), wakisubiri taratibu za ujazaji fomu za kujiunga katika Chuo cha Mafunzo ya Ufundi(VETA) jijini Dar es salaam, hivi karibuni.
Ujazaji fomu za kujiunga na masomo ya ufundi VETA ukiendelea. Vijana hawa ni miongoni mwa vijana 11 wanaofadhiliwa na Help for Underserved Communities Inc. (HUC).
Baadhi ya vijana walipata ufadhili wa masomo ya ufundi toka Help for Underserved Communities Inc. (HUC), wakijaza fomu za kozi mbalimbali walizoomba VETA, jijini Dar es Salaam hivi karibuni. Kutoka kulia ni Monica Mhelela, Joseph Mboya na Hassan Bakari.
Jamila Mwenda na Joseph Mboya wa Dar es Salaam, wakionesha nyuso za furaha baada ya ndoto zao za kusomea usekretari kwa Jamila na ufundi magari kwa Joseph kutimia. Jamila na Joseph ni miongoni mwa vijana 11 wanaofadhiliwa na Help for Underserved Communities Inc. (HUC)
tunawashukuru kwa kuwasaidia vijana wetu mungu awape moyo huo mzidi kutusaidia
ReplyDelete