Msanii wa muziki wa kizazi kipya kutoka kundi la TMK Wanaume "Chege "akionyesha umahiri wake wa kutawala jukwaa wakati wa Tamasha la Cheka Bombastiki lililofanyika katika ufukwe wa Coco beach jijini Dar es Salaam mahususi kwaajili ya wateja wa Vodacom na uzinduzi wa simu za mkononi za Huawei kwaajili ya wateja wao wakati huu wa sikukuu ya Krismasi.
Msanii wa kundi la Tiptop Connection Madee akiwaburudisha mamia ya wakazi wa jiji la Dar es salaam waliofurika katika ufukwe wa Coco Beach, wakati wa kusherehekea sikukuu ya krismasi na kuzinduliwa kwa simu za mkononi za Huawei ,wakati wa Tamasha la Cheka Bombastik lililoandaliwa mahususi kwaajili ya wateja wa kampuni hizo.
Msanii nguli wa muziki wa kizazi kipya Profesa Jay akiwapagawaisha mashabiki waliofurika katika ukumbi wa Dar Live uliopo Mbagala jijini Dar es Salaam, wakati wa Tamasha la Cheka Bombastik lililoandaliwa na Vodacom Tanzania na Serengeti kwaajili ya wateja wao wakati huu wa msimu wa sikukuu ya krismasi.
BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI
BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...